Mfumo wa Uuzaji (Marketing) umebadilika zaidi katika miaka mitano iliyopita kuliko miaka 50 iliyopita, na maendeleo haya ya haraka sana hayaonyeshi dalili zozote za kushuka kwa mfumo huo.

Mpaka kufikia 2019, mazingira ya uuzaji/utafutaji wa masoko kwa njia ya kigiditali (Digital Marketing) ambayo yanajumuisha SEO, Mitandao ya kijamii, PPC, Content marketing yanazidi kushuhudiwa madiliko yake makubwa mno.

Mitindo na mikakati mingi mipya ya uuzaji wa kwa njia ya kidigitali inaibuka katika enzi ya sasa ya hali ya juu, iliyounganishwa na mtandao, ambayo inamaanisha kuwa biashara zinahitaji kuzitumia njia hizo ili kufanikiwa katika biashara zao kwa sababu kile kilichofanya kazi mwaka jana kinaweza kisifanye kazi mwaka huu.

SOMA ZAIDI:

Njia bora za Digital Marketing ambazo haupaswi kuzipuuzia (Digital Marketing Trend)

1.   Akili za bandia (Artificial Intelligent-AI)

Matumizi ya akili za bandia sasa ndio kitu pekee ambacho kinaenda kutawala duniani. Hizi utumika katika kurahisisha kazi tu. Kwa mfano Microsoft na Uber au Taxify.

Sehemu kama viwanja vya michezo, Maduka makubwa ya bidhaa, huwa wanatumia roboti kwa ajili ya kuweka mazingira ya usalama n ahata wakati mwingine kuuza bidhaa. Wakati mwingine roboti hawa uweza kusoma hata namba za magari, kuripoti matukio yenye shaka kwa wahusika.

Vitu vingine ambavyo hutumia akili za bandia (Artificial Intelligent) ni pamoja na Chatbots ambayo utengeneza mfumo wa malipo yaani Master card.

2.   Chatbots

Chatbots itabaki kuwa sehemu muhimu sana katika digital marketing katika miaka ya hivi sasa. Huu ni mfumo ambao unapokea na kutoa ujumbe kupitia facebook Messenger.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wateja wengi wanaupendelea huu mfumo kwa kiasi kikubwa sana, na kama wafanyabiashara watautumia mfumo huu unaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwenye bajeti yao.

3.   Video Marketing

Huu ni mfumo ambao ndio gumzo na habari mjini kwa sasa n ahata kwa miaka 5 hadi 1o ijayo. Asilimia kubwa sana ya wafanyabiashara sasa husambaza video za biashara zao kwa kiasi kikubwa mno. Na wengi wao wanakiri kuwa njia hiyo imeleta matokeo makubwa ukilinganisha na njia zingine walizotumi.

Lakini hata wateja sasa wanaamini sana kwa kile wanachokiona. Wateja wanakuwa huru kufanya manunuzi kwa bidhaa waliyopata kuona kwa njia ya video. Utafiti uliofanywa na kampuni ya Single Grain ulibain kuwa zaidi ya 52% ya wateja wanasema kuwa kuangalia bidhaa mkwa njia ya video inawapa uhuru wa kufanya manunuzi ya mtandaoni.

4.   Matumizi ya watu wenye ushawishi (Influencer Marketing)

Hii ni aina ya uuzaji ambayo inalenga sana kuwatumia watu mashuhuri au maarufu kufikisha ujumbe kwenye kundi kubwa la watu. Kikubwa cha kuzingatia watu hawa maarufu wawe wanatumia Instagram au Youtube tena wenye wafuasi (followers) wa wengi.

Mfano, nchini Tanzania wanamuziki wengi wamekuwa ndio jukwaa la kutangaza biashara mtandaoni kutokana na umaarufu wao na kuwa na wafuasi wengi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

5.   Matumizi ya programu za Mitandao ya kijamii kutuma ujumbe. (Social Messaging App)

Kama ulidhani matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii basi ni kutumiana ujumbe na emoji na marafiki zako basi unakosea. Idadi kubwa ya watumiaji wa mitandao hii unaweza kuibadilisha na kuwa watu wanaokuingiza kipato.

Kuna zaidi ya meseji bilioni 10 zinatumwa Duniani kila mwezi kupitia mtandao wa facebook. Wakati huo huo zaidi ya watu bilioni 1.6 wanatumia mtandao wa whtasap kila siku na zaidi ya meseji bilioni 55 zinatumwa kila siku kupitia mtandao huo. My brother hii ni takwimu kubwa sana ambayo watu wa masoko hasa kupitia mtandao hawawezi kuipuuzia.

Mitandao hii inaweza kutumika kutuma meseji za masoko moja kwa moja kwa mteja kwa ajili ya kufikisha taarifa, kutambulisha bidhaa, kutoa na kuomba mawasiliano, kualika kwenye matukio mbalimbali ya kibiashara.

6.   Marco-moments

Huu ni wakati ambapo tunapoingia kwenye vifaa vyetu vilivyounganishwa na mtandao kama vile simu, kompyuta n.k kwa ajili ya kufanya matendo Fulani kuhusiana na “nini tunahitaji?” (What we need) na “nini tunataka” (What we want).

Mara nyingi mtu mwenye ndiye anayefanya maamuzi ya nini angependelea kula, na atakula kwenye hotel gani, bei zake zikoje au wapi pengine pa kwenda.

Hivyo basi watu wa masoko wanahitaji kujua

·        Ninahitaji kwenda…..(I want to go)

·        Ninahitaji kujua……..,(I want to know)

·        Ninahitaji kufanya……(I want to do Moment)

·        Ninahitaji kununua………(I want to buy moment)

Hili kuweza kuendana na mfumo huu unahitaji kujua wapi walaji wanatumia kutafuta (search) taarifa kama hizo, ikiwa ni google basi unapaswa kutumia platform hiyo.

7.   Social Media Story

Mtandao wa SnapChat umekuja na kipengele cha “My story” na baadae Facebook na Instagram wakatambulisha mfumo huo kabla ya Youtube nao kufanya hivyo.

Kipengele hiki kinaleta ufanisi kwenye biashara kwa kiasi kikubwa kama kitatumiwa kwa mantiki ya kibiashara.

Kiujumla zipo njia nyingi ambazo hazipaswi kupuuzwa katika zama hizi hasa katika upande wa kutafuta masoko. Mustakabali wa digital Marketing bila shaka unabadilishwa na teknolojia. Kwa msaada zaidi wa kufahamu jinsi ya kutumia njia hizi au kwa namna nyingine Deep Media wanakupa nafasi ya pekee sana. Bonyeza HAPA kwa mawasiliano.