Kulingana na ongezeko kubwa la watumiaji wa mtandao (Internet). Ni wazi mashirika, makampuni, watu binafsi na hata biashara mbalimbali, hawapaswi kukaa mbali na platform hiyo kama wanahitaji kujulikana kwa walaji au watumiaji wake. Hii ni kwa ajili ya kukuza jina lake, iwe kwa biashara au isiyo ya biashara (Brand awareness).

Ripoti ya TCRA ya mwezi Machi, 2019, inaonyesha kuwa, utafiti uliofanyika mwaka 2018, zaidi ya 43% ya watu wote nchini Tanzania wanatumia internet, ambao ni zaidi ya watu Milioni 23,142,960. Hili ni ongezeko la 3% ukilinganisha na 40% ya mwaka 2017.

Duniani kote kulingana na ripoti ya mwezi Juni, 30, 2019, inaonyesha kuwa zaidi ya 57.3% ya watu wote Duniani wanatumia internet. Ambao ni zaidi ya watu bilioni 4.4.

SOMA ZAIDI:

Matumizi ya internet Platform katika kukuza jina la kampuni/biashara

Ongezeko kubwa la watumiaji wa Matndao/internet ni fursa kubwa kwa kila mtu kuweza kuitumia kwa ajili ya kutengeneza mtandao mkubwa wa kibiashara na hata kijamii. Kwa kutumia internet ni wazi unaweza kufikisha ujumbe kwa watu wengi na kwa muda mfupi na kwa haraka pia.

Changamoto kubwa iliyokuwepo sasa hasa nchini Tanzania. Licha ya idadi kubwa ya watu wanaotumia internet kuongezeka mara dufu, bado makampuni, mashirika na hata mashirikisho hayajalichukua hilo kama fursa ya kujitangaza na kujikuza.

Na ndio maana sio jambo la kushangaa hii leo kukuta kampuni au shirika au hata shirikisho halina hata tovuti (website), mtandao wowote wa kijamii au kitu chochote kinachomuunganisha na mtandao/internet.

Tunategea hii leo unapokuwa unatafuta kampuni Fulani kupitia mtandao, vitu kadhaa vitajidhihirisha, mfano

  1. Logo (nembo ya kampuni au shirika)
  2. Picha za matukio mbalimbali
  3. Viunganishi vya kurasa za Mitandao ya kijamii kama kampuni/shirika inatumia
  4. Viunganishi vya matukio mbalimbali (Events)
  5. Anuani

Faida za kuunganishwa na mtandao

  1. Urahisi wa kufikisha taarifa au huduma/bidhaa mpya

Kampuni au shirika linapounganishwa kwenye mtandao tunategemea kuwa litakuwa limejitengenezea njia nyepesi ya kufikisha taarifa au ujumbe kwa walaji wake.

  1. Kukuza jina la kampuni/shirika

Unapokuwa na kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii au tovuti. Kuna uwezekano mkubwa wa maudhui yako kuonekana mara kwa mara kwenye mtandao. Hali inayopelekea maudhui hayo kubaki kwenye vichwa vya watu.

  1. Kuongeza Idadi ya wafuasi kwenye kampuni/shirika lako

Mtandao unakuweka karibu sana na jamii au hadhira inayokuzunguka. Kadri unapokuwa unatumia mtandao kwa ufasaha kufikisha taarifa au kuelezea jambo kwa jamii inakutengenezea nafasi ya kuwa chanzo tegemevu kwa watu.

Hizo ni baadhi tu ya faida ambazo unaweza kuzipata. Fikiria katika idadi ya watu Milioni 23.1 wanaotumia mtandao Tanzania, ni wangapi wanajua au wanafahamu shughuli za kampuni/shirika lako?

Au ni wangapi walikutafuta mtandaoni kwa kutumia jina la kampuni yako lakini hawakufanikiwa kuona japo logo ya kampuni yako? Na ni mara ngapi umefikiri kuwa wateja na watumiaji wa huduma zako wapo kwenye kundi hilo la watu milioni 23.1 ambao wanatumia internet?

Bado haujachelewa, Deep Media digital Agency in Tanzania imetoa ufumbuzi wa maswali hayo kwa makampuni mengi nchini, na sasa yameunganishwa na mtandao na kuwaweka karibu na wateja wake. Kwa ajili ya kupata ushauri juu ya msuala ya kidigitali yote lakini pia kuunganishwa na mfumo wa digitali unaweza kuwasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA. Au kwa kupiga simu kwa nambari 0758259234