Maisha ya biashara sasa yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana. mteja hahitaji huduma za kienyeji au kiasili sasa. Watu wanaweza kupata majibu ya maswali yao wakiwa mtandaoni. Na kama ukishindwa kuwasaidia kwa jinsi wanavyotaka na kwa haraka basi watatafuta njia au sehemu nyingine.

Sasa ni wazi wateja wanapokwa na jambo Fulani zaidi ya nusu yao watatafuta ufumbuzi mtandaoni. Daima utafuta majibu ya maswali yao yaliyo bora na kwa aharaka sana na yaliyo rahisi kuyapata.

Kama itatokea wanafanya mawasiliano na biashara yako, zaidi ya 70% kati yao watataka ujue wao ni nani na hawatakuwa tayari kurudiarudia kutoa taarifa zao. Ikitokea una bahati basi unaweza kujikuta unapata ushirikiano mzuri.

Lakini ikitokea umeshindwa kutimiza matakwa yao hasa kutoa huduma kwa ufanisi basi ni rahisi kwao kuwashirikisha wengine kupitia mitandao ya kijamii kuhusu hasira yao.

SOMA ZAIDI:

Ukweli kuhusu wateja wa biashara yako

1.Wateja huwa wanahitaji kujisaidia wenyewe kabla ya kukupigia wewe mwenyewe.

Daima wateja wa sasa wanapokuwa na shida ya kitu chochote uenda kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kwenye mtandao. Huwa wanaamini kuwa majibu ya maswali yao yatapatikana huko.

Hivyo basi mteja anaamini mara tu atakapotembelea mtandao atapata jibu ambalo anaona litamsaidia katika matatizo yake. Lakini anapokosa msaada huisi kuwa mtandao husika umekosa kitu cha kuaminika.

Mteja anapenda sana kujihudumia mwenyewe kuliko kuanza kutengeneza cheni ya biashara baina yake na mfanyabiashara.

2.Mteja huwa anajifunza kupitia kwa marafiki zake na sio kwa wauzaji.

Mara nyingi mteja hasa watumiaji wa mitandao upenda kugawana taarifa kuhusu jambo Fulani liwe baya au zuri. Mteja anapopata huduma au anapokuwa amefanikiwa au ameshinda kutatua tatizo lake ni rahisi sana kuwashirikisha marafiki kwa kile kilichokuta.

Marafiki ni wajumbe wazuri wa biashara yako. Mteja huwa anapenda kujifunza kwa rafiki yake aliyepata huduma au kununua bidhaa Fulani kuliko kwa muuzajiwa bidhaa.

3.Mteja anapenda kuamini kwa wateja wengine na sio mikakati yako ya masoko

Mara nyingi wateja huwa wana tabia ya kugawana taarifa. Biashara yako inapofanya vizuri basi hata mteja atakuwa mjumbe mzuri wa biashara yako. Wateja huwa wanaaminiana wenyewe kwa wenyewe kuliko watu wa masoko.

Mabadiliko haya yanazidi kusonga mbele kwa kasi huku maendeleo ya teknolojia yakionekana kuchangia kwa kiasi kikubwa. Maendeleo ya teknolojia yamefanya kuwa rahisi kwa mtu kupata taarifa anaozitaka kwa haraka na urahisi mkubwa.

Sio jambo la rahisi kwa makampuni kukubali mabadiliko haya ila ili kuweza kukua makampuni yanapaswa kuzingatia haya. Mteja anachangia kwa kiasi kikubwa kwa ukuaji wa biashara yako.

·Mteja ataipendekeza kampuni yako kwa marafiki zake wengine.

·Atashuhudia mafanikio yake kwa watu wengine ulimwenguni kote kupitia mtandao.

Ni wazi sasa maendeleo ya teknolojia yamekuja na changamoto chanya hasa kwenye ulingo wa kibiashara. Makampuni yanahitaji kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye kutengeneza wateja ambao watakuwa wajumbe kupitia mitandao mbalimbali.

Unaweza kupata ushauri wa kibiashara na hata kukunganisha katika kurasa zenye kuleta tija katika biashara yako kwa kubonyeza HAPA.