Sio siri tena kuwa soko la muziki linazidi kukua siku hadi siku nchini Tanzania na hata Duniani kiujumla. Mfumo wa njia za mauzo sasa umehama kutoka kwenye mfumo wa taslimu au wa uuzaji wa CD hadi kwenye mfumo wa kimtandao.

Wapo baadhi ya wasanii nchini Tanzania sasa ufanya mauzo ya muziki wao kwa njia ya mtandao hii huwasaidia kukuza soko la muziki wao na hata kujitengenezea mashabiki wengi ulimwenguni kote.

Wanamuziki kama Diamond Platnum na Alikiba wamekuwa wakiingia makubaliano na makampuni mbalimbali ya kuuza muziki mtandaoni Duniani. Hii ni ishara kubwa sana kuwa soko la muziki linazidi kukua ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

 

       SOMA ZAIDI:

 

 

Mbinu za kukuza muziki wa Tanzania kupitia mfumo wa digitali

  • Matangazo ya moja kwa moja ya Muziki (Live music promotion)

Kwa kutumia njia za kidigitali kukuza soko la muziki ni rahisi kusahau mfumo wa ana kwa ana. Msanii anaweza kutengeza wimbo na ukautambulisha kupitia mtandao na ukaenda katika mawanda mengi na hatimaye wapenzi wake wakaupakua wimbo huo.

  • Matumizi ya mitandao ya kijamii.

Idadi kubwa ya watu wanatumia mitandao ya kijamii, iwe facebook, Instagram na hata twitter. Msanii anaweza kutumia mitandao hii kukuza soko la muziki wake. Mitandao ya kijamii sio soko la moja kwa moja bali inatengeneza soko kubwa la muziki. Instagram sasa imekuwa sehemu kubwa ya kujenga soko la muziki. Hakikisha vitu unavyoviweka kwenye kurasa vinakuwa vyenye kufurahisha kwa 80% huku 20%  vyenye maudhui ya kuutangaza muziki.

  • Kutangaza muziki kwa kuuza kupitia Tovuti.

Hili kuwaweka mashabiki na wapenzi wa muziki wako Karibu na msanii, matumizi ya ni bora zaidi. Tovuti inaweza kusaidia kama njia ya kukuza soko la muziki kwa asilimia kubwa. Tovuti itatumika kuuzia tikiti za maonyesho yote msanii atakayoyafanya  kwa mwaka, kuuza album na muziki kiujumla

  • Tumia blogu za muziki kutengeneza hadhira mpya.

Suala la kukuza muziki sio tu kusambaza nyimbo zako bali unapaswa kutenegeneza wasikilizaji wapya na kuwabadilisha kuwa mashabiki wako. Hili kukuza soko la muziki wako unahitaji blogu ambayo huwa inaweka maudhui mapya na yenye kupendwa na watu. Na mtu ambaye atakuwa ameipenda blogu atakuwa anakuona mara kwa mara.

Fanya utafiti kujua ni blogu gani zinajishughulisha sana na masuala ya muziki kwa kiasi kikubwa.

  • Kushirikiana na wasanii wengine

Muziki wa kushirikiana umepata sifa ya kukuza soko la muziki ulimwenguni kote. Ni njia nzuri sana ya kuufanya muziki wako ufike katika mawanda mapana sana. Jaribu kushirikiana na wasanii ambao tayari wana akiba kubwa wa wafuasi na mara unapoisambaza video yako kwenye mtandao wa Youtube ipate kuwa na wafuatiliaji wengi walioitazama.

 

  • Matumizi ya akaunti ya Youtube.

Ili kuweza kupanua soko la muziki wako matumizi ya youtube vi vigumu kuweza kuyaepuka. Sasa hivi nchini Tanzania wasanii wengi utumia ukurasa huu kwa ajili ya kusambaza video zao kwa mashabiki zako na kupata kipato kutokana na idadi ya wafuatilia au wafuasi walioitazama video husika.

 

  • Kuingia makubaliano na makampuni ya kuuza muziki mtandaoni.

Makampuni kama Apple music, iTunes, Sonny, Universal pamoja na Mkito yanaingia mikataba mbalimbali yenye kusaidia kukuza soko la muziki Duniani. Kwa kufanya kazi na makampuni kama haya kunatengeneza soko la muziki katika eneo kubwa.

Ni wazi sasa ili muziki wa Tanzania uweze kupenya na hatimaye soko la muziki wake liwe kubwa ni vigumu kutenganisha na matumizi ya digitali. Wapo baadhi ya wasanii kama vile Diamond Platnum tayari ameshafanya mauzo ya album yake kupitia mtandao.

Zipo njia nyingi za kutengeneza soko la muziki na kuweza kupenya kwenye mawanda makubwa.Unaweza kubonyesha hapa kuona jinsi gani unaweza ukatumia mtandao kukuza muziki hata biashara yako.