Mabadiliko ya teknolojia ulimwenguni ni dhana adhimu iliyokuja kwa ajili ya kusambaza taarifa anuwai kwa njia ya mtandao. Taarifa ambazo zitaleta mbadiliko chanya katika maisha ya kila siku ya binadamu. Mabadiliko haya ni muhimu sana kutokea kwa ajili ya ustawi mzuri wa mandeleo katika eneo Fulani.

Duniani kote makampuni mengi sasa yanaangazia mabadiliko haya ya teknolojia au digitali mbayo yameleta mapinduzi katika Nyanja ya kibiashara kwa kutengeneza aina ya bidhaa na huduma mpya ambayo itaingia kwenye soko la ushindani.

SOMA ZAIDI:

Je, Unajiuliza smartphone inawezaje kukusaidi kwenye biashara yako?

Hivi unajua kuwa smartphone (simu ya mkononi) inaweza kukusaidia kuendesha na kukuza biashara yako?  Je unadhani smartphone ni kwa ajili ya mitandao ya kijamii pekee? Ngoja nikueleze kidogo.

Smartphone inakupa nafasi ya kufanya vitu vingi sana kwa wakati na mahali popote. Unaweza kuitumia kwa kuendesha tovuti ya baishara yako, kuangalia barua pepe zako, kusikiliza muziki, kufanya mawasiliano binafsi na hata kupiga picha ama kuangalia video mbalimbali.

Kwa taarifa tu wafanyabiashara wengi ulimwenguni sasa wanaendesha biashara zao kupitia simu ya mkononi. Lakini tatizo kubwa linaloipa changamoto njia hii ya kutumia smartphone ni uwepo wa vingele (features) au App ambazo smartphone haiuwezi kumiliki yenyewe.

NJIA ZA KUTUMIA SMARTPHONE KATIKA BIASHARA

  • Tenganisha matumizi ya simu zako, ya biashara na matumizi binafsi
  • Pakua App itakayokupa uwanja mpana wa biashara yako
  • Tengenza mpangilio rahisi wa APP ya biashara kwenye simu yako
  • Tengeneza mfumo au sera sahihi ya mawasiliano hasa kwa watakaohitaji kuwasiliana na biashara yako.
  • Tumia mifumo ya sauti kufikisha ujumbe wa wateja wako
  • Unganisha barua pepe ya biashara yako na simu yako.
  • Ongeza baadhi ya dhana za simu yako zinazoweza kukupa urahisi wa matumizi ya simu yako.
  • Tambua mpiaka yako ya kufanya biashara na simu yako ikiwemo kujua muda gani unapaswa kuzima simu yako au kuwasha simu yako.
  • Zipangilie App za simu yako ambazo muhimu mbele ys uso wa simu yako ili uweze kuzitumia na kuzipata kwa urahisi.
  • Suala la usalama liwe kipaumbele hasa katika App na vingele vyote unavyovitumia kwenye simu yako. Epuka kuchanganya matumizi binafsi na biashara katika simu ya biashara.

Smartphone inaweza kukupa urahisi wa kuendesha biashara yako lakini unahitaji kuwa na APP yenye uwezo wa kuipa biashara yako thamani.

FAIDA ZA KUWA NA “MOBILE APP”

  1. Inatoa thamani kubwa ya biashara yako kwa wateja wako

Biashara siku zote ni mfumo wa kupeana, wewe unamuuzia bidhaa au huduma yeye anafungua pochi yake.

Unaweza kukaa chini na kufikiria njia zaidi ya mteja kuendelea kufungua pochi yake zaidi. Njia ya kutengeneza mwingiliano zaidi na mteja wako ili kuongeza mauzo. Kwa kuwa na matumizi ya APP unaweza ongeza thamani kwa mteja wako kwakuwa mteja anaweza pata huduma popote anapokuwa.

  1. Inajenga uimara wa Jina la biashara yako (Build a Stronger Brand)

Moja ya vitu vinavyotolewa kwenye App ya biashara yako kwa mteja wako ni ufahamu wa jina la biashara yako kwa ufasaha. Pamoja na mawasiliano yote ya biashara yako.

Hii inatengeneza uaminifu kwa wateja wako. Zaidi wateja wako wanavyoonesha uaminifu wa biashara yako ndio zaidi watakavyohitaji kusikia zaidi kuhusu bidhaa au huduma yako mpya.

  1. App inawaunganisha vyema wateja wako.

Huduma kwa wateja kwa sasa ni zaidi ya mawasiliano ya ana kwa ana. Zaidi ya watu bilioni 2.6 sasa wameunganishwa na mtandao wa simu za mkononi hivyo App za simu zimekuja kubadilisha aina ya ufanyaji wa biashara kwa wateja.

  1. App ya simu inakuza faida ya biashara yako.

Kama hali ya utoshelezaji kwa mteja au uridhishwaji kwa mteja utaongezeka bila shaka na mauzo yataongezeka pia. Kulingana na takwimu za salesForce, 70% ya uzoefu wa ununuaji unatokana na jinsi gani mteja najihisi anapokuwa napatiwa huduma.

Kadri mwenye maslahi na biashara yako au mteja aliyepatiwa huduma kwa ufasaha anapokuwa ndio bidhaa yako na biashara yako ndivyo kiasi kikubwa cha wahitaji wa bidhaa yako kitaongezeka.

  1. App ya simu inawezesha kumpa taarifa mtumiaji kuhusu bidhaa na ofa mpya.

Matumizi ya App za simu kwa biashara urahisisha mfumo mzima wa mzunguko wa biashara yako. Inaweza kumpa mtumiaji ujumbe wenye kuonyesha uwepo wa biadhaa au ofa mpya ya biashara yako.

Kulingana na takwimu za ComScore, matumizi ya App za simu kwenye biashara imekuwa kwa zaidi ya 50% katika kipindi cha miaka 2 iliyopita.

Unaweza sasa na wewe kuanza kutumia App  ya simu kwa ajili ya biashara yako kwenye simu yako ya mkoni. DEEP MEDIA wanakupa nafasi ya wewe kumiliki App yenye uwezo wa hali ya juu na vingele vyenye kuleta tija kwenye biashara yako kulingana na ushauri wa kitaalamu.