ZINGATIA:

Katika ulimwengu ambao biashara ya mtandaoni inakua kwa kasi sana kupeleka bidhaa yako kwenye maonyesho ya kibiashara pamoja na matamasha inaweza kuonekana kama mbinu iliyopitwa na wakati katika kukuza biashara yako.

Ukweli ni kwamba kufanya maonyesho ya bidhaa au huduma yako kwenye maonyesho au matamasha bado inakuza mauzo kwa kiasi kikubwa.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya 82% ya wateja wanaoudhuria maonyesho ya biashara huwa wanahusika moja kwa moja katika kufanya maamuzi ya kununua bidhaa au huduma katika maonyesho, hivyo kufanya kuwa njia bora ya kukuza mauzo ya biashara yako.

Maonyesho ya biashara yanaweza

  • Kukuunganisha na wafanyabiashara wengine ambao mnafanya biashara ya aina moja.
  • Kukuza jina la biashara yako kwa wateja wengi zaidi
  • Kukuwezesha kupata mrejesho wa biashara yako kwa urahisi.

Ili kuweza kushiriki mauzo ya biashara kwa ufanisi katika banda la maonyesho ya biashara tunakuleta mbinu 5 za kuuza biashara yako katika banda la maonyesho.

  • Wavutie waudhuriaji wa maonyesho kwa bidhaa bora na zenye kuvutia.

Kwenye sehemu yenye mkusanyiko wa mabanda ya biashara tofauti tofauti unahitaji sekunde chache tu kuweza kumvutia mteja ili aweze kufika na kuhitaji bidhaa au huduma yako.

Unaweza kutumia michezo mbalimbali, muziki wa kuvutia, video, kutoa ofa tofauti tofauti kama vile chakula na vinywaji. Uwepo wa ubunifu wa mbinu za masoko kama hizo unatengeneza mazingira ya furaha kwa wateja na hivyo kuweza kupokea idadi kubwa wa wateja.

READ MORE: MIMI NNI MFANYABIASHARA MDOGO. JE NAHITAJI TOVUTI?

  • Lenga makampuni na wafanyabiashara wengine waliohudhuria.

Hii ni njia nyingine ambayo unaweza kuvutia watu wengi kusogea kwenye banda lako. Tumia ubunifu mkubwa kuwavutia makampuni washiriki wa maonyesho.

 

 

Mfano unaweza kutengeneza utaratibu maalumu wa masoko kwa kutengeneza njia nzuri ya kupima, kuchambua utendaji kazi wa tovuti na kurasa za kibishara za mtandaoni,  kuonyesha kwenye moja ya runinga zenu kubwa zilizopo kwenye maonyesho ili kuweza kuwavuta washiriki wenza.

  • Uza uzoefu na sio bidhaa

Watu wengi uhusudu kitu kutokana na mazoea ama uzoefu wa kitu husika, kwa sababu ana uzoefu ama mazoea na kitu hicho ama jambo Fulani, hivyo huwa kama utambulisho wake.

Kama unakuja na bidhaa au huduma ambazo watu wamekuwa sehemu ya bidhaa au huduma hizo basi unaweza tengeneza idadi kubwa ya watu kwenye banda lako.

Mfano kampuni moja ya maji iliamua kutengeneza maji safi kwenye maonyesho ya biashara kwa ajili ya jamii ya watu wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea, hivyo kila mtu aliyepita aliweza kupewa chombo chenye ujazo wa maji na kutembea nacho yadi 50 kama wale waishio vijijini wafanyavyo.

 

 

  • Hakikisha mashine ya kadi ya malipo inafanya kazi vizuri.

Kwa kipindi hiki cha karibuni watu wengi upendelea kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki au kadi ya malipo. Hakikisha mfumo wa ulipaji wa kieletroniki unafanya kazi ipasavyo.

Kuweka mfumo wa ulipaji wa taslimu pekee utakufanya upoteze fedha nyingi kwa watu wengi ambao hawalipi kwa fedha taslimu.

READ MORE: HOW I MADE A FORTUNE USING SOCIAL MEDIA

  • Muhudumie mtu yeyote anayekuja kwenye banda kama mteja wa malipo

Unapofanya maonyesho huwa kuna wateja tofauti tofauti:-

  • Mteja wa kutaka kujua zaidi kuhusu huduma au bidhaa unayouza
  • Mteja wa malipo ambaye huwa na lengo la kununua bidhaa au huduma

Muhudumie mtu yeyote anayekuja kwenye banda lako bila kujali ni aina gani ya mteja. Jibu maswali ipasavyo.

Kwa kuzingatia utaratibu huo unaweza kuvutia wateja wengi kwenye banda lako la maonyesho,

sio tu wateja toka nje pia unaweza kuvutia makampuni shiriki kutokana na ubunifu utaounyesha