Hakuna shaka kuwa leo YouTube imekuwa ndio sehemu maalum ya kuangalia video mbalimbali kama ilivyokuwa Google katika miaka ya nyuma. Kwa hakika Youtube sasa ni “Search engine” ya pili kwa ukubwa Duniani ikiwa na watu zaidi ya bilioni 1,8 waliojisajili kwenye tovuti hiyo ya kuangalia video ambayo kila siku uangaliwa video zaidi ya bilioni 5.
Uwepo wa Channel za YouTube mbalimbali na matumizi yake makubwa umebadilisha kabisa upepo wa matumizi ya televisheni za asili. Wimbi kubwa la watu ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa wanatumia televisheni za kawaida sasa wamehamia kwenye televisheni za Youtube ambapo uuwezesha kutazama popote alipo na kile anachohitaji kutazama.
Rekodi za YouTube
- Idadi ya Viewers wa You Tube kila siku Duniani ni zaidi ya watu Milion 63 kwa mujibu wa mtandao wa Youtube
- Idadi ya Viewers wa You Tube kila mwezi Duniani ni zaidi ya Milioni 149 kwa mujibu wa mtandao wa statista
- Zaidi ya 50% ya watumiaji wanatumia kupitia simu za mkononi (Ripoti ya YouTube)
- Video ambayo imetazamwa sana mpaka sasa ni “Despacito” yenye zaidi ya watazamaji bilioni 6.
- Mapato yaliyokadiriwa kwa mwaka 2015 yalikuwa zaidi ya dolla bilioni 8
SOMA ZAIDI:
- Smartphone inavyoweza kukusaidia katika biashara yako
- Jinsi ya kukuza biashara yako kupitia mtandao
- Siri nzito kuhusu masoko mtandaoni
Kiujumla Youtube imekuwa na matokeo makubwa sana kwa kipindi cha karibu mara baada ya kutokea kwa mapinduzi teknolojia ambapo tunashuhudia idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet inazidi kuongezeka siku hadi siku. Idadi pia ya watu wanaotumia simu za mkononi ambao ni zaidi ya 50% ya wanaotazama video za Youtube inaongezeka.
Watu wengi sasa wamekuwa wakifikiria kuanzisha televisheni za Youtube lakini tatizo kubwa limekuwa ni kutokuwa na uelewa wa jinsi gani wanaweza kuingiza fedha kupitia Youtube.
Swali kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni
“Ni watazamaji (viewers) kiasi gani unaweza kutengeneza fedha kwenye You Tube”?
Hii ni swali la kawaida na linaloulizwa mara kwa mara na inategemea nani anauliza. Huenda umesikia kwamba unaweza kutengeneza dola moja kwa viewers elfu moja au kwamba ni dola 1,000 kwa kila viewers Milioni. Wengine wanasema ni dola 5 kwa viewers elfu moja. Hapa unauliza swali lisilofaa.
Kwa bahati mbaya kulingana na matakwa ya Youtube hauwezi kutengeneza fedha unayoitegemea kwa kutegemea tu Idadi ya watazamaji ulionao.
Bali utatengeneza pesa kulingana na ushiriki wa watu kwenye matangazo (Based on People’s engagement with the Ads). Ushiriki hapa inamaanisha kubonyeza (Clicking) au kutazama tangazo kwa sekunde zaidi ya 30. Matangazo ya Youtube usimamiwa kwenye jukwaa la Adwords. Watangazaji (Advertisers) huchagua matangazo aidha kwa Gharama kwa kila unapobonyeza (Cost Per Click) au Gharama ya kila unapotazama (Cost Per View).
Aina za Matangazo (Types Of Ads)
-
Utoza Gharama kwa kila unapobonyeza (Cost Per Click)
Ni aina ya tangazo ambapo mtangazaji hutozwa gharama kulingana na idadi ya watu waliobonyeza (number of Clicks). Mfano tangazo limeonyesha alama (Keyword) ya CPC ni dola 3 basi mtangazi atatozwa dola 3. Mara nyingi ni matangazo yanatokea kwenye uso channel ya Youtube mara unapofungua.
-
Hutozwa Gharama kutokana na kila unapotazama (Cost Per view)
Hapa mtangazaji (Advetiser) analipa gharama kulingana na idadi ya watazamaji. Hapa hamaanishi wale waliotazama video iliyoko kwenye You Tube bali idadi ya watu waliotazama tangazo lililoko hata kwa sekunde 30. Haimaniishi kuangalia mara kwa mara itamchaji mtangazaji mara nyingi bali inatoza mara tu unapoliangalia kwa mara ya kwanza.
Zingatia haya yote hufanyika mara baada ya akaunti yako ya You Tube kuipeleka kwenye mfumo wa kifedha/kibishara (Monetarization). Na mfumo huu unakuruhusu pindi tu utakapofikia idadi Fulani ya watu waliokufuata au kujiunga na mtandao wako wa Youtube (Subscribers)
Njia nyingine zinazoweza kukuingizia fedha kupiti You Tube.
- You Tube Partnership Program
- Merchandising
- You Tube Super chat
- Crowdfunding
- Sponsored Videos
- Affiliating Marketing
- You Tube Premium
Ni wazi sasa kama ulikuwa unafikiria kuanzisha You Tube yako basi utakuwa unajua kwa jinsi gani unaweza ingiza kipato kupitia YouTube. Kwa Msaada kuhusu kuendesha biashara yako au kukuza biashara yako kupitia mfumo wa kidigitali wasiliana na Deep Media kwa KUBONYEZA HAPA.