Je! Una mtandao mkubwa na watu? Je, una portifolio iliyojaa mafanikio ya wateja wako? Inawezekana kuwa ni kweli unahitaji kuwa mshauri (Consultant), lakini inakuwa vigumu kwako kujua uanzie wapi.
Deep Media digital Agency Tanzania, imekuwa ikiandaa semina mbalimbali zinazohusiana na masuala mablimbali. Wiki hii imepata nafasi ya kuendesha semina maalumu ya “Jinsi ya kuwa mshauri” yaani “how to become a Consultant”
Je, Mshauri (Consultant) ni nani?
Huyu ni mtu ambaye ni mjuzi kwenye sekta fulani, ambaye utoa ushauri wa kitaaluma kwa watu lakini hata kwa wafanyabiashara kulingana na uwanja wake aliobobea.
Kwa maana nyingine Mshauri (Consultant) ni mtu ambaye anatoa ujuzi wake wa kipekee kwenye taasisi au kwa mtu fulani. Unaweza kuwa mshauri kwenye masuala ya:
- Kibiashara
- Mauzo
- Masoko
- Fedha/Uhasibu
- Teknolojia
- Sheria
- Mahusiano ya Umma (Public relatios)
Je, wewe una eneo lolote ulilobomea kitaaluma? Na je, umeshawahi kufikiria kutaka kuwa mshauri wa eneo hilo ulilobobea?. Ni rahisi sana.
Jinsi ya kuwa Mshauri (How to become Consultant)
Kuwa mshauri ni dhana moja. Lakini pia kuwa malengo ni dhana nyingine. Kuwa mshauri inategemea unalenga nini hasa. Lakini kiujumla kuwa mshauri kutakusaidia
- Kuongeza kipato (To increase income)
- Kutatua kesi mbalimbali kwa vitendo
- Kuongeza ujuzi kwenye taaluma yako.
Aina za washauri/Consultants
-
Mshauri wa ndani (Internal Consultant)
Huyu ni mtaalamu ambaye anaajiriwa kwa muda wote na shirika, ambaye anaripoti kwa meneja mkuu au usimamizi mwingine. Yeye anafanya kazi pekee ndani ya uwanja wa shirika aliloajiriwa lakini pia kwa ombi la meneja ambaye anaripoti.
-
Mshauri wa nje (External Consultant)
Ni mtaalamu ambaye hafanyi kazi ndani ya kampuni mama au kampuni ya kuajiriwa. Ni mtaalamu ambaye ana ujuzi katika eneo fulani na hutoa huduma zake kwenye sekta ya umma au binafsi.
Malengo ya Mshauri
- Kuanzisha uhusiano chanya
- Kutatua matatizo
- Kuhakikisha kunakuwa na umakini kwa tatizo la kiufundi / biashara na uhusiano
Mshauri (Consultant) anapaswa kuwa na ujuzi gani?
Mshauri/consultant anapaswa kumiliki baadhi ya ujuzi au taaluma itakayomuwezesha kwenye kazi yake. Baadhi ya taaluma hizo ni pamoja na
I. Ujuzi wa kiufundi (Technical skills)
Hapa mshauri anapaswa kuwa na uwezo wa matumizi ya muda (Time management), uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja kama timu (team work) pamoja na ujuzi wa kutumia baadhi ya softaware.
II. Ujuzi wa kushirikiana na wengine (interpersonal Skills)
Mshauri anapaswa kuwa mwerevu kifikra hasa katika kukubali mawazo mapya (Open Minded), kusaidia, pamoja na kuheshimu.
III. Ujuzi wa kushauri (Consulting skills)
Hapa tunazungumzia ujuzi wa kujenga uaminifu, kusikiliza, pamoja na kujenga hoja kwa ufupi na kwa kiungwana.
Baada ya hapo kipi unapaswa kufanya (Way Forward)
- Badilisha CV yako kuwa mawanda mapana
- Anzisha tovuti yako na barua pepe iliyo rasmi (Formal e-mail)
- Tengeneza mfumo wa taarifa zako na anza kuwasiliana
- Tembelea kwenye mikutano ya mauzo (sales meeting)
- Andika maombi (Proposal) na jitahidi kuomba zabuni mbalimbali
- Sasa furahia mkataba wako wa awali.
Kwa msaada zaidi ili kuweza kushiriki kwenye semina mbalimbali zinaozendelea au hata kuingia kwenye mfumo wa kidigitali ambao utaifanya biashara yako kutoka hapo ilipo na kusogea mbele. Tafadhali bonyeza HAPA au wasiliana nasi kwa simu nambari 0758259234