Unafahamu bila ya kuwa na ukurasa wa mteja wa mawasiliano hauwezi kutengeneza mteja kwenye biashara yako ya mtandaoni?
Ukurasa wa mteja ndio sehemu lengwa ya kumvuta na kumshawishi mteja. Lengo maridhawa la ukurasa huu ni kumtaka mteja ajaze taarifa zake kutokana na maudhui aliyoyapitia kwenye ukurasa husika.
Kutokana na kuwa ukurasa huu ni sehemu muhimu kwa kumvuta mteja unapaswa kubuniwa kwa umaridadi wake.
Vipengele vitano (5) vinavyounda Ukurasa bora wa Mteja
- Ukurasa wa mteja unapaswa kuwekwa sehemu yenye kuonekana kwa urahisi.
Mteja anapotembelea ukurasa wako kusoma maudhui mbalimbali ahitaji mpaka afike mwisho wa ukurasa. Weka ukurasa wa mteja juu pembeni au chini ya tovuti ili aweze kuufikia kwa haraka.
- Urefu wa Fomu ya mteja
Swali kubwa la kujiuliza ukiwa unaandaa fomu ya ukurasa mteja ni kwa ukubwa gani inapaswa kuwa?
- Urefu na ufupi wa Fomu
Urefu na ufupi wa fomu unatumika katika kupata idadi na ubora wa taarifa za kwenye ukurasa wa mteja. Fomu inavyokuwa fupi ndivyo unapokaribisha wateja wengi kuacha taarifa zao kwa urahisi. tofauti na fomu iliyo ndefu.
Fomu yenye maelezo machache itakupa idadi ya wateja wengi. Lakini haitakupa ubora wa taarifa. Fomu ndefu itakupa wateja wachache nyenye ubora wa taarifa.
SOMA ZAIDI:
- KAMPUNI ZINAZOTENGENEZA TOVUTI KWA BEI RAHISI
- JE? MFANYABIASHARA MDOGO ANAHITAJI TOVUTI?
-
Matakwa ya mteja kujaza fomu.
Kawaida mteja anaepuka sana kujaza fomu zenye maelezo marefu. Epuka kuweka maelezo marefu na kuomba taarifa nyingi kwenye ukurasa wa mteja.
-
Vipengele vya maswali kwenye fomu.
Bila shaka swali litakuwa vingele vya maswali kwenye fomu vitakuwaje?. Taarifa gani nitaziulizia kwenye ukurasa wa mteja?. Mara nyingi kampuni uulizia taarifa nyingi kwenye tovuti zao. Jitahidi kukusanya taarifa za kutosha kadri iwezekanavyo ili kupata mawasiliano muhimu na mteja wako. Hii inajuimsha,
-
Vipengele vya kumchanganua mteja
-
Kuuliza maswali ambayo ni ya umuhimu tu.
-
Sera ya Usiri
Wateja wengi huwa wanapata hofu unapoulizia taarifa zake muhimu sana. Unapaswa kumfanya mteja ajenge imani na wewe na taarifa zake muhimu anazozitarajia kuzitoa. Weka sera ya usiri katika hali ya kiusalama. Unaweza kutumia vyeti vya usalama au utepe wa dhamana (guarantee seal) kwenye ukurasa wa mteja.
-
Kitufe cha kuwasilisha Taarifa
Mteja anapomaliza kujaza taarifa zake kwenye ukurasa wa mteja unapaswa kumuonyesha kitufe cha kuwasilisha taarifa zake mara tu atakapomaliza kujaza.