Kama unatumia mtandao wa Instagram, utakuwa unajua ni furaha kiasi gani kuona followers, likes na comments zako zinavyoongezeka. Ni wazi kila mtu anayetumia mtandao huu basi ni fahari kwake kuona ukurasa wake ukishamili kwa idadi ya watu wanaotoa maoni na hata kufollow kila wakati.
Kwenye andiko hili leo nataka upate elimu kidogo kuhusiana na mtandao wa Instagram na takwimu zake zinavyoweza kukukuza kibiashara. Hapa tunazungumzia Instagram insights.
Instagram Insights ni nini?
Hiki ni kipengele au mfumo wa ufuatiliaji wa takwimu za muhimu/asili za akaunti ya mtandao wa Instagram. Unaweza kutumia mfumo huu (Instagram insights) kujua au kuwatambua wageni kwenye akaunti yako. Unaweza pia kutambua ni aina gani ya maudhui (content) wanayopendelea zaidi. Lakini pia inaweza kukusaidia kuchambua kwanini post nyingine zimefanya vizuri zaidi kuliko nyingine. Na mwisho kukupa njia za kuweka mikakati thabiti ili uweze kuwapa hadhira (audiences) yako kile wanachohitaji na kutarajia.
Sehemu muhimu za uchanganuzi wa Instagram Insights (Metrics)
Unaweza ukadhani kuwa kuchambua takwimu za Instagram ni kazi ngumu mno inayofanywa na watu waliobobea kwenye hisabati. La asha, ni rahisi mno. Insights inatumia njia rahisi mno ya kutoa takwimu zake kwa kuwa tu inatoa namba zilizo kwenye maelezo yenye kuelezea maana halisi. Hivyo basi hata kama ulikuwa unafanya vibaya kwenye somo la takwimu (statistics) hapa hauwezi kufanya vibaya tena. Instagram imegawanya takwimu zake katika makundi 3, nayo ni
-
Takwimu za account (Account insights)
Account insights inatoa taarifa zote za kitakwimu zinazohusiana na akaunti yako ya Instagram (Business account) katika makundi 3
-
The activity tab
Hapa inaonyesha kwa jinsi gani watu wavyojishughulisha kwenye akaunti yako. Kama vile idadi ya watu wapya (nuw visitor) na kama walibonyeza kwenye links yako yeyote au kwenye mawasiliano yako. Inakuonyesha pia idadi ya watu walioifikia/kuiona post yako katika kipindi cha siku 7.
Hapa unaweza ukaona ni jinsi gani unaweza ukajipima na kujilinganisha na washindani wako kibiashara. Hii itakusaidia kuongeza au kupunguza baadhi ya vitu ili uweze kuwafikia zaidi wateja wako.
-
The Content tab
Sehemu hii inaonyesha utendaji kazi mzima wa post uliyoweka, matangazo, stori mbalimbali. Hii itakusaidia wewe kuchanganua ni post gani imefanya vizuri zaidi kuliko nyingine. Hii itakusaidia kukupa mawazo katika kuboresha kwenye post zako kibiashara zaidi.
-
The audience tab
Hapa inakuonyesha maelezo ya audiences/followers wako katika makundi mbalimbali kama vile jinsia, mahali walipo, umri, kazi n.k. hii itakuasaidia katika biashara yako ili uweze kuwafikia au kufikia kundi ulilolikusudia.
-
Takwimu za Post (Posts insights)
Ili kuweza kuona takwimu hizi kwenye post unapaswa kubonyeza kwenye sehemu iliyoandikwa “View Insights” chini ya post yako. Hapa utaona taarifa mbalimbali kama vile likes, comments, forwards na save your post.
Kipengele cha Forward and save kinakusaidia wewe kujua ni kwa kiasi gani audiences wamesave post kwa ajili ya kuiangalia baadae, au kwa ajili ya kusambaza kwa rafiki zao wengine.
-
Takwimu za Stori (Story insights)
Kwa kubonyeza kwenye Tab ya Instagram Story, unaweza kuona idadi ya watu ambao wameona (view) stori uliyoichapisha. Hapa ndipo pia unaweza kuona ni watu wangapi wameandika chochote kuhusu stori uliyochapisha.
Kumbuka ili uweze kupata taarifa zote hizi (Instargram insights) lazima akaunti yako ya Instagram iwe imewezeshwa kwenye akaunti ya biashara (Instagram Business account). Na hakuna gharama za kuifanya akaunti yako ya Instagram kuwa ya biashara (business account).
Ili uweze kupata maelezo zaidia au kupata ushauri wa juu ya matumizi sahihi ya Instagram na mitandao mingine kibishara. Tafadhali wasiliana nasi, Deep Media digital agency moja kwa moja kupitia nambari za simu 0758259234,