Tarehe 14, Februari kila mwaka Dunia huwa inaadhimisha siku ya wapendanao (Valentine’s Day). Bila shaka ni siku inayoibua hisia kubwa kwa watu mbalimbali ulimwenguni. Hata hivyo, watu wenye mawazo ya biashara wanaangalia fursa za ujasiliamali za kupata pesa katika siku hiyo.

Mambo muhimu zaidi ni kuwa na ubunifu na kuwa na uhalisia. Siku hii watu wengi hutumiana zawadi. Haijalishi zawadi ya aina gani, iwe ya kuhamishika au la. Utegemea na uwezo na nafasi ya mtu kwahiyo kila kitu au biashara inategemea na mazingira husika.

Kama ulikuwa unafanya biashara Fulani unapaswa kujua aina ya wateja wako. Je wateja wako ni waanaume au wanawake? Je vipi kuhusu umri wao? Soko la biashara la siku ya wapendanao mara nyingi huendana na umri wa wateja wako.

Valentine’s day ni nini?

Kimsingi, siku ya valentine ni siku ya wapenzi au wapendanao. Siku hiyo pia inajulikana kama Siku ya “Saint Valentine” au Sikukuu ya Saint Valentine. Katika siku hii, wanandoa au wapendanao hupeana zawadi, chocolates, kadi na bouquets za maua. Na wanafurahia siku pamoja na shughuli nyingi za kujifurahisha.

Zaidi ya hayo, katika miongo ya hivi karibuni siku ya wapendanao imeongezeka na kuwa siku ya kibiashara na tukio maarufu la kutoa zawadi. Kimsingi, Matangazo ya Siku ya Wapendanao yanawahimiza wanandoa au wapendanao kutumia wakiwa pamoja. Kwa hakika, ni fursa kubwa kwa wajasiriamali ambao wanataka kutengeneza pesa nyingi katika siku hii. 

SOMA ZAIDI:

Vitu vinavyoweza kukupatia kipato siku ya Valentine

1.     Utengenezaji wa Chocolate

Hakika kama una ujuzi wa kutengeneza chocolate nzuri na tamu, hii ni fursa kwako ya kutengeneza pesa siku ya valentine. Hata, unaweza kufikiria kuanza biashara hii kutoka jikoni kwako. Kwa kawaida, kuna njia kadhaa unaweza kuuza chocolates kwa wateja wako.

Hata hivyo, biashara nzuri inahitajika ili kupata mafanikio katika biashara hii. Watu wengi upenda kununua chocolate katika siku hii kwa ajili ya kuwapelekea wapendwa wao. Hivyo unaweza kuamua kutengeneza na kuziuza katika njia mbalimbali. Kama vile kupita kwenye maofisi mbalimbali ukiwa umezifunga kwenye furushi maalum.

2.     Biashara ya kuki (Cookies)

Cookies ni zawadi nzuri na kamili kwa ajili ya tukio la Siku ya Valentine. Ikiwa wewe unataka kuanza biashara ya kuki na unataka  kuwekeza mtaji mdogo wa biashara yako basi hii ndio biashara sahihi kwako. Uuzaji wa biscuits na bites nyinginezo unaweza ukawa na faida nzuri katika siku hii ya wapendano kwani wengi wao upenda kutumiana kama zawadi.

3.     Kutengenza Duka la Maua/ Uuzaji wa Maua

Bila kujali kuwa unabiashara ya maua ama la. Unaweza kuanzisha duka la maua au biashara ya maua kwenye siku ya wapendanao. Kimsingi, maua ni vitu maarufu sana ambavyo karibu kila wanandoa au wapendanao ununua wakati huu. Kulingana na uwezo wako wa uwekezaji, unaweza kuzingatia uuzaji kwenye mtandao au kwa kawaida. Biashara hii inaweza ukuingizia kipato kikubwa sana siku hii.

4.     Utenegenzaji wa Kadi mbalimbali (Greeting Cards Making)

Kimsingi, kadi za salamu na za za kutakiana heri ni vitu vingine maarufu kama zawadi ya Siku ya Valentine. Siku hii ndugu, jamaa, marafiki na hata wapendanao huwa wanatumiana kadi mbalimbali kuonyesha iashara ya upendo. Hivyo basi utengenezaji wa kadi mbalimbali unaweza kukupa nafasi ya kuingiza kipato ikiwa tu utazitafutia njia nzuri ya kuzisamabaza. 

5.     Kuuza zawadi za binafsi (Personalized Gift selling)

Ikiwa wewe ni mtu wa ubunifu mwenye mawazo chanya ya kutafuta masoko ya biashara , basi unaweza kufikiria kuanzia biashara ya kuuza zawadi ya kibinafsi. Kwa kweli, zawadi za kibinafsi ni zawadi maalum kwa mtu ambaye ni maalum sana. Unaweza kuendesha biashara hiyo kutoka kwenye duka la rejareja na mtandaoni. Watu wengi upenda kutengenezewa zawadi ao binafsi na kupelekewa pale walipo. Hili ni wazo zuri la kibiashara na kuingiza kipato. 

6.     Biashara za safari za furaha (Travel related Business) 

Siku ya wapendanao, wanandoa na wale wapendanao wanaangalia aina tofauti za ziara zenye vifurushi vizuri. Na unaweza kutengeneza pesa nyingi kwa kuwasaidia. Kwa ujumla, unaweza kugawa ziara zako kwa makundi mawili. Usafiri wa ndani na wa kimataifa.

Sekta ya usafiri na utalii wa U.S. huzalisha zaidi ya dola 1.5 trillioni katika pato la uchumi siku hizi. Wapendanao wengi upenda kubadilisha mazingira katika siku hii kwa kutembelea sehemu mbalimbali. Unaweza kuanzisha biashara ya kuwapeleka wapendanao sehemu ambayo unahisi wanaweza kupata utulivu na kuingiza kipato.

Mbali na orodha hii ya mawazo ya biashara, kuna fursa kadhaa ambazo zinaweza kukufaa zaidi. Hii kutokana na ujuzi wako, uzoefu na uwezo wa uwekezaji, unapaswa kuchagua biashara sahihi ambayo unaweza kuanza siku ya Valentine.

Ili kuweza kujua unawezaje kuifanya biashara yako kupitia njia ya kidigitali. Deep media wanakukutanisha na jopo la wataalamu wa masuala ya biashara hasa katika mfumo wa kidigitali ili kuongeza thamani ya biashara yako. Bonyeza HAPA kwa mawasiliano zaidi.