Kuna msisimko mkubwa kuhusu teknolojia mpya katika huduma kwa wateja, msaada, na mafanikio. Maendeleo ya video, ujumbe wa muda halisi, mazungumzo na akili ya bandia (AI), matumizi ya fedha kupitia mtandao (cryptocurrencies), huduma binafsi, na hata mafanikio ya wateja yenyewe.Vyote hutoa uwezekano wa mabadiliko makubwa katika kazi za kila siku kwa watendaji au watoa huduma kwa wateja.
Lakini uwepo wa teknolojia mpya unakuja na changamoto, pia. Kunatakiwa na uhitaji mkubwa wa kujifunza ili kuweza kutumia na kukabiliana na teknolojia hiyo mpya. Inaweza kuwa na gharama kubwa kutekeleza, na kuna wasiwasi unaokuja kuhusu teknolojia mpya: Je, inakuja kuiba kazi zetu?
Jibu fupi ni hapana. Teknolojia nyingi mpya zitatumika tu kusaidia wataalamu wanaojitokeza kwa wateja kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. Teknolojia hizi zinaweza kubadilisha kazi yako. Hata hivyo na ndio maana utabiri huo wa kupoteza kazi umeingia.
SOMA ZAIDI:
- The best 5 Personalization Software Option 2019
- 10 Tips for successful customer-client relation management
Kwanini teknolojia inatishia kazi ya huduma kwa wateja?
1. Mawasiliano ya picha mjongeo (Video) ya ana kwa ana yataongezeka
Mawasiliano ya ana kwa ana huwa yana nguvu sana. Wateja zaidi na zaidi, wataona kuwa njia isiyo ya video na mazungumzo ya sauti halisi kama kitu cha zamani na kilichopitwa na wakati. Makampuni mengi sasa hutumia njia ya mawasiliano ya video kwa ufanisi zaidi kama vile “Video Voicemail” kama mkutano kwa njia ya video
Tunajua kwamba mawasiliano ya jicho (ana kwa ana) yanaboresha uhusiano na kuwezesha uwazi (ikiwa ni katika biashara au katika maisha yako binafsi). Hivyo njia ya video si tu matarajio yanayoongezeka ya watumiaji, lakini zana inayofaa ya kuboresha biashara kwa wauzaji. Unapaswa kuanza kutumia Video Voicemali sasa. Lakini pia mikutano iliyopangwa na wateja inapaswa kuhusisha mkutano wa uso kwa uso wakati wowote iwezekanavyo.
2. Huduma ya kujitegemea (Self-service) itakuwa ni ya lazima kabisa.
Tangu mara ya kwanza mtu alipoandika mwongozo wa mtumiaji (User manual) huduma ya kujitegemea ilikuwepo. Lakini kwa maana zaidi, wateja na watumiaji wanabadilka kwa haraka sana na wanatarajia fursa zaidi za huduma za kibinafsi kuliko hapo za hapo awali.
Kwa nini mabadiliko hayo yanatokea? Wafanyabiashara wengi ambao watumiaji wake wa bidhaa huingiliana katika biashara wameunganishwa na teknolojia ya kisasa. Fikiria kuhusu Amazon, Facebook, Google, Walmart, wauzaji wakuu, mabenki makubwa na kadhalika.
Biashara hizi kubwa zinatumia huduma ya kujitegemea kwa sababu inapunguza gharama zao za kufanya biashara. Lakini kwa kufanya hivyo, wao pia wanasukuma bahasha kwa mbinu za kisasa zaidi za mwingiliano wa wateja. Baada ya muda, biashara ambazo haziwezi au haziendani na mabadiliko haya zitaonekana kama zimepitwa na wakati kwa watumiaji wa wastani.
Fikiria ulimwengu ambako unashirikiana mara kwa mara na “messenger bots” au programu za simu za kutambua mahali. Ungefikiri ni ajabu sana ikiwa biashara haikutoa njia hizi za kujitegemea, na kukulazimika kutumia kitu cha zamani kama simu au barua pepe.
Hatua ya kwanza ya kusaidia wateja wako ni kujisaidia wenyewe? Unahitaji msingi wa maarifa ambapo unaweza kuandika majibu kwa maswali ya kawaida ya wateja ambayo wanaweza kupata kwenye Google au kutumia vifaa vyao vya kutafakari sauti mara kwa mara .
-
Mafanikio ya mteja ndio kitakuwa kipimo cha ushindani
Zaidi ya miaka mitano ijayo. Mafanikio makubwa ya wateja yatakuwa faida kubwa ya ushindani kwa makampuni, kama msaada mkubwa wa wateja ni leo. Sekta ya mafanikio ya mteja, na maendeleo ya makampuni katika kutafuta thamani ya wateja, ni ya haraka sana na ya ufanisi kwa hii kutokea.
Uwepo wa teknolojia itakayomsaidia mteja kupata huduma au bidhaa anayoitaka kwa wakati tutakuwa tunahesabu kama moja ya mafanikio, hivyo kuleta imani kwa wateja.
-
Huduma kwa wateja itatoka na mfumo wa data.
Bila kujali teknolojia ya huduma unayochagua, inapaswa kujumuisha njia ya kupima mafanikio yake kwa kiasi kikubwa. Bila hivyo, hakuna njia ya kuthibitisha kama programu iliyoongeza in ufanisi wowote. Hivyo, kama makampuni yanaendelea kutumia teknolojia ya huduma, timu zao za huduma za wateja zitategemea zaidi kuchambua mafanikio ya programu hizi.
Pamoja na mabadiliko hayo, lazima iwe na mvuto mkubwa wa data muhimu inayozunguka katika idara zote za huduma za wateja. Teknolojia ya huduma hurekodi taarifa mbalimbali kuhusu ushirikiano wa wateja ambao hutumiwa kutambua mahitaji ya wateja yanayopuuzwa au yenye vikwazo.
5. Mitandao ya kijamii itakuwa ndio chombo cha huduma kwa wateja
Mitandao ya kijamii imewawezesha watumiaji wake kuwa na uwezo wa kukosoa mara kwa mara biashara fulani mtandaoni. Mapokeo mabaya ya huduma au bidhaa kwa mteja yanaweza kurekodiwa na kuwekwa mtandao na kuonekana na mamilioni ya watumiaji wa mtandao.
Takwimu zinasema zaidi ya 83% ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wana uwezekano wa kuamini maoni ya wenzao, hii inaweka shinikizo kwa timu za huduma za wateja ili kuja na mpango thabiti na ufanisi wa majibu.
Kwa kufanya hivyo, makampuni yatapaswa kubadili akaunti zao za mitandao ya kijamii kushughulikia hali za huduma kwa wateja. Hii ina maana kuwa njia za Mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, na Instagram zitakuwa chaguo bora kwa wateja ambao wanatafuta kuwasilisha maoni.
Ni wazi sasa ujio wa teknolojia mpya unakuja na changamoto hasi na chanya. Wapo wanaoamini kuwa ujio wake unakuja kupunguza nafasi za ajira. Lakini wapo wanaoamini kuwa ujio wake utakuja kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma kwa wateja.
Kwa msaada zaidi wa jinsi ya kupata Mobile App zinazoweza kuendesha biashara yako, kampuni yako wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.