Mfumo wa kibiashara sasa unabadilika kwa kasi, ni wazi hata watu wa masoko nao wanajaribu kuendana na mfumo mpya wa uuzaji na ununuzi wa bidhaaa/huduma. Hakuna shaka kwenye zama hizi za kisasa kuona kuwa sehemu kubwa ya mikakati ya masoko ni matumizi ya mfumo wa kidigitali. Walaji pamoja na wafanyabiashara kwa pamoja daima hushinda mtandaoni. Na moja ya mikakati ya kimasoko ni kusoma tabia za walaji wanapokuwa wanatumia mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii imeshika soko zima. sasa unaweza kuuza na kununua kwa urahisi zaidi kupitia mitandao hii.
Kukiwa na zaidi ya watumiaji bilioni 2.4 wa facebook kila mwezi. Lakini pia zaidi ya watumiaji bilioni 1 wa Instagram kila mwezi, kama mfanyabiashara umeshawahi kujiuliza unawezaje kutumia takwimu hizo na kuzibadilisha kuwa fedha?
Unawezaje kutumia mitandao ya kijamii kuzalisha wateja?
Wapo wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii pasipo kujua ni njia zipi au mambo gani wanapaswa kufanya ili kuweza kuzalisha wateja kwenye biashara zao. Mitandao ya kijamii inaweza kutumika kama platform kubwa ya kukuza biashara yako kwakuwa ukiwa na unatumia mitandao ya kijamii unaweza,
-
Kuandaa kampeni mbalimbali za mauzo kwenye biashara yako
Matumizi ya kampeni kupitia mitandao ya kijamii mara nyingi huzingatia lengo kuu la kampeni. Unaweza ukaamua kufanya kampeni kwa ajili ya kupata wateja moja kwa moja. Au kupata wateja ambao wanaweza kuacha mawasiliano yao ili uweze kufanya nao biashara.
Faidia kubwa ya kampeni hizi inakupa wigo wa kuchagua ni wateja wenye umri gani, wanaotoka maeneo gani na katika vipengele vingine.
-
Kutumi Link za biashara kusambaza kwenye mitandao ya kijamii
Wapo wanaodharau matumizi ya link mbalimbali zinazokuwa zinasambazwa hasa kwenye makundi mbalimbali ya kwenye mitandao ya kijamii. Lakini ukweli ni kwamba Link zina uwezo wa kusambaa kwa watu wengi zaidi na hivyo kukufanya kupata wateja zaidi.
-
Kutumia Mitandao kama sehemu ya kuweka matangazo yako ya kibiashara.
Unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kutengeneza na kusambaza matangazo yako ya kibiashara. Daima wale ambao wanavutiwa na biashara yako basi watakutafuta pale watakapohitaji. Kikubwa matangazo yakidhi vigezo ikiwemo uwepo wa anuani ya mawasiliano ya baishara yako.
Zipo njia nyingine kama vile kuandaa mashindao kupitia mitandao ya kijamii, matumizi ya webinar au live video n.k
Deep Media digital Agency wamesaidia makampuni na biashara mbalimbali katika kuhakikisha idadi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa eneo husika inaleta tija kwenye eneo la kibiashara.
Tupigie 0758259234