Unatumia mitandao ya kijamii? Si ndio? Au? Na kama ni ndio, ni mara ngapi umeshawahi kufikiria kwa jinsi gani unaweza kuitumia mitandao hiyo kuimarisha kazi yako? Bila shaka sio mar azote umekuwa ukifikiria hilo. Chukua mfano wa mtandao wa Instagram, mara nyingi umekuwa ukitumia mtandao huu kupost, kulike picha pamoja na kushare picha zile zinazokuvutia.

Naomba utambue hili, zaidi ya mitandao mingine yote, Instagram inatoa nafasi kubwa mno kutengeneza brand ya mtu au biashara na hata kampuni. Tambua kujenga brand yako mwenyewe iliyo imara sio jambo muhimu sana kwenye biashara yako bali ni muhimu sana kwa ajili ya kuwavutia watu sahihi kwako kama wateja wa biashara yako kwa siku za usoni.

Jinsi ya kujibrand kupitia Instagram

Hakuna kitu chochote chenye kuwafikia hadhira kubwa ambacho hakina mipango iliyo sahihi. Instagram pia, ili uweze kufanikiwa kutengeneza jina lako au hata jina la biashara yako ni vema ukafuata baadhi ya kanuni na miongozo ili uweze kufanikiwa. Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo unaweza kuzitumia ili uweze kujibrand kupitia Instagram.

  1. Andaa mipango iliyo thabiti

Jambo la kwanza unalotakiwa kulifanya ni kuweka mipango iliyo thabiti ili uweze kutimiza lengo lako. Mipango hiyo inajikita kwenye

  • Malengo na madhumuni yako (Goals & objectives)

Lazima utambue ni kitu gani ambacho unataka ufanikiwe kupitia akaunti yako ya Instagram. Kujua malengo yako itakupa nafasi nzuri ya kujua ni maudhui gani utatumia kwenye akaunti yako.

  • Hadhira lengwa

Watu ambao unahitaji kuwafikia (Target) itakupa wakati mzuri wa kujua ni aina gani ya maudhui ya kupost.

  • Wasifu uliobora (Profile)

Tengeneza wasifu ulio bora ili uweze kumvutia hadhira yako

  1. Tumia njia bora kujibrand (Brand it well)

Kama utakuwa unajua brand yako basi ni rahisi kujibranda. Unapaswa kujijua kwanza wewe mwenywe, wewe ni nani?  Umetokea wapi? Ili uweze kuja na njia iliyo bora ya kutengeneza attention kwa hadhira yako.

  1. Matumizi ya Hashtag (Don’t forget to hashtag)

Hashtag ina nafasi kubwa sana katika kujitambulisha kwa hadhira yako. Hashtag inakutambulisha vyema kulingana na maudhui unayoyapendelea kuyapost. Hii itakusaidia kupata engagement kubwa kulingana na hashtag ya maudhui yako.

  1. Sambaza maudhui/akaunti yako (Share)

Akaunti zote maarufu za Instagram mara nyingi zinakuwa za watu walio maarufu kwenye jamii. Kutumia watu wenye ushawishi kwenye jamii yako kwa kusambaza maudhui au akaunti yako kwao inaweza kuwa njia nyingine ya kujibrand kwako.

  1. Muda wa kushiriki kwenye maudhui yako na hata mengine mtandaoni (Keep engaging)

Mitandao ya kijamii inaweza kuwa na changamoto, hasa kwenye suala la muda. Unapaswa kuwa kwenye mtandao wa Instagram wakati wote ili watu wengine waweze kukuona. Jitahidi kupost hata mara moja kwa maudhui yenye kuvutia huku ukiendelea kucomment na kulike maudhui mengine.

Akikisha katika madhui yako unazingatia

  • Mahali (Location)
  • Picha iliyo bora (Image)
  • Maelezo na maneno yaliyo mafupi na kueleweka (Caption & text)
  • Call to action
  • Hashtag

Haya ni baadhi ya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine kama utayazingatia basi utaweza kujibrand vizuri. Msaada zaidi, tembelea tovuti ya Deep Media Digital agency HAPA au wasiliana nasi kupitia namba zetu za simu 0758259234 ili tuweze kukusaidia wewe pamoja na biashara yako.