Mitandao ya kijamii imebadilisha kabisa jinsi tunavyoishi maisha yetu kwa sasa. Kutoka kwa njia zinazotupatia habari zetu za kila siku na kwa jinsi tunavyowasiliana na wapendwa wetu. Mitandao ya kijamii sasa imeenea kila mahali. Haiwezi kuepukika, imekuwa na nguvu kubwa mno.

Tangu mwaka 2004, Mitandao ya kijamii ilikuwa imeongezeka kwa kiasi kikubwa na lakini ilikuwa haijafikia kilele cha umaarufu wake bado. Hakuna anayeweza kukataa kwamba majukwaa ya mitandao ya kijamii sasa ni chanzo kikuu cha habari na Mawasiliano.

Lakini swali ni, Je, kuna thamani ya kuwekeza biashara yako katika mitandao ya kijamii? Je, masoko ya mitandao ya kijamii yanapaswa kuwa eneo la lengo la mkakati wako wa masoko mwaka 2019?

Takwimu za mitandao ya kijamii za 2019 zinaonyesha kuwa kuna watumiaji wa mitandao ya kijamii zaidi ya bilioni 3.2  Duniani kote, na idadi hii inakua tu siku hadi siku.

Tayari sasa unaweza kujua jinsi mitandao ya kijamii ilivyo ya muhimu kwa kuongeza uelewa wa bidhaa yako, kuzalisha wateja wa biashara yako zaidi, na hatimaye kubadilisha kabisa biashara yako.

SOMA ZAIDI:

Faida za kujitangaza kupitia Mitandao ya kijamii

  1. Si ya gharama, inaweza kufikiwa na mfanyabiashara yeyote (Affordable)

Dhna na Program mbalimbali za mitandao ya kijamii ni nafuu mno. Na Vifaa/programu nyingi za mitandao ya kijamii ni bure. Kutangaza kupitia mitandao ni rahisi mno ukilinganisha na njia za kawaida tulizozizoea. Lakini pia inaweza kukupa matokea hata zaidi ya njia ambazo ungezitumia kwa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha.

  1. Inakuza ufahamu wa biashara yako kwa haraka na urahisi zaidi

Mojawapo ya faida kubwa ya mitandao ya kijamii ni uwezo wake wa kuongeza ufahamu wa bidhaa/biashara yako kwa haraka (to increase brand). Kutumia mitandao ya kijamii kwenye biashara yako kunakupa nafasi ya kujitambulisha kwa wateja/walengwa wa biashara yako kwa haraka zaidi na mawanda mapana kwa kulinganisha idadi kubwa ya watumiaji wa mitandao hiyo ya kijamii ambayo ni zaidi ya bilioni 3.2.

  1. Ni rahisi kutumia (Easy to use)

Kutumia mitandao ya kijamii ni rahisi sana na pia ni rahisi kujifunza kwa mtuamiaji wa awali. Mitandao ya kijamii ni rafiki sana hivyo una uwezo wa kutumia popote ulipo endapo tu utakuwa na kifaa kinachokuwezesha kupata mitandao ya kijamii.

Wkati mwingine matumizi ya mitandao ya kijamii unaweza kujifunza kupitia mitandao ya mbalimbali kama vile tovuti na na majukwaa mbalimbali.

  1. Kuendana na washindani wako kibishara

Bila kujali ni sekta gani au lengo kuu la soko lako ni nani, kuna nafasi nzuri ya kuwa washindani wako tayari wamejiunga na mitandao ya kijamii. Hii sio tu inaonyesha kuwa kuna fursa ya wewe kufanya vizuri kwenye mitandao hii, lakini inamaanisha kwamba baadhi ya wateja wako wanaweza kuwa tayari kuzungumza kuhusu ushindani uliopo baina ya mshindani wako.

Ikiwa unataka kubaki kwenye ushindani katika soko la digital, ni muhimu kwamba uanze kufanya kazi ya kujenga uwepo wako kwenye jukwaa hilo. Maudhui ya mitandao ya kijamii hayakuwezeshi kuonyesha tu uzuri wa biashara yako lakini pia inatoa ufanisi wa shughuli zako pamoja na ujuzi wako.

  1. Inaokoa Muda

Matumizi ya Mitandao ya kijamii yanaokoa muda ukilinganisha na njia nyingine katika kuitangaza biashara yako. Unaweza kuamua kutumia mitandao ya kijamii wakati wowote ule utakaoona unafaa. Hivyo basi haikupi masharti ya muda na wakati maalumu wa kuyaendesha matangazo yako.

Mitandao ya kijamii pia inakuwezesha kuelewa vizuri zaidi jinsi tabia za wateja wako mtandaoni. Kwa mfano, unaweza kutumia jukwaa la analytics kwenye Facebook ili uone ni aina gani ya maudhui pendwa kwa wateja wako.

Deep Media inakupa nafasi sasa ya kujipambanua kwa wateja wako kupitia mitandao ya kijamii. Ambapo sasa tunakupa fursa ya kuitangaza biashara yako kwa ajili ya matokea chanya. Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA au wasiliana nasi moja kwa moja kupitia 0689055415.