Wamiliki wawili wa biashara marafiki siku moja waliambatana kwenda kupata vinywaji kwenye kilabu kimoja cha pombe. Wote wawili waliagiza toti za kilevi kusherehekea mafanikio ya kuanzisha kampuni mpya kila mmoja.
Miaka 5 baadae wafanyabishara hao walikutana tena kwenye kilabu kile kile cha awali na kuagiza kama ilivyo kawaida yao. Baadae mmoja alimgeukia mwenzake na kumueleza kuwa ameajiri mfanyakazi wake wa 25. Yule mwingine alikuwa anendelea tu na kilevi ghafla akamgeukia na kumuambia kuwa amesaini nyaraka za ufirisi wa biashara yake hivi karibuni.
Huu sio utani, ni stori ya kweli, tunachopaswa kujua kutoka kwa wafanyabiashara hawa wawili ni utafauti wao mkubwa wa mikakati ya biashara zao.
Yule wa kwanza yeye alitengeneza tovuti ya biashara siku ya kwanza tu baada ya kuanzisha kampuni ili kuendana na soko la kisasa, wakati yule wa pili yeye alitegemea tu kutumia mitandao ya kijamii pekee. Somo ni kuwa usiwe kama mfanyabiashara wa pili.
Tovuti ni nini?
Ni mkusanyiko wa kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakilishi kama vile HTML, PHP, XHTML na kadhalika na ambazo kwa pamoja hujumuika katika kutoa maudhui ya muundo tofauti tofauti kwa kutumia picha mnato, picha mjongeo, maneno, sauti ikitambulishwa na jina maalum la wavuti yaani Domain name.
- Tovuti 5 bora zinazoweka matangazo ya Ajira
- Sababu 5 za kwanini unahitaji Tovuti mpya 2019
- Je? unahitaji mauzo zaidi? fuata hatua hizi.
Sababu 5 za kampuni ndogo kumiliki Tovuti
- Uaminifu(Credibility)
Kampu ni ndogo inahiataji kujenga uaminifu kwa wateja wake. Lakini sio tu kujenga uaminifu kwa wateja wake laini pia tovuti inafanya biashara yako kukua na kujulikana kwa haraka zaidi.
- Kukuza jina la Biashara
Watu wanapofikiria kuhusu jina la biashara au kampuni wanafikiri kuhusu nembo ya kampuni au biashara pekee lakini ni zaidi ya hapo. Jina la biashara ni chombo kikuu cha biashara ni kile ambacho mtumiaji wa huduma na bidhaa ufikiria wakti wote. Sio tu kwa ajili ya kufanya biashara yako kujulikana bali kumfanya mtumiaji wa huduma au bidhaa za kampuni yako kuelewa kuhusu biashara yako na hata kujenga uaminifu.
- Suala la Masoko.
Dhama za matangazo ya kwenye mbao na matangazo ya radio zinazidi kupungua kwa kasi. Kadri mtumiaji wa mtandao anapoingia mtandaoni ukutana na tovuti mbalimbali zenye taarifa tofauti. Biashara ndogo inahitaji kujiwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye suala la masoko ili kukuza biashara.
- Ushindani
Ushindani wa kibiashara ni wazi sasa umehamia kwenye mtandao. Biashara nyingi sasa zimewekeza kwenye kuanzisha kurasa mbalimbali mtandaoni kujitangaza. Baadhi ya kampuni ndondogo wamejikita kuanzisha kurasa mbalimbali ni wazi kwa kampuni ndogo ambazo haijawekeza kwenye masoko ya mtandaoni hasa kwa kurumia tovuti yatashindwa kushindana nay ale yaliyowekeza kwenye masoko ya mitandaoni hasa kwa kutumia tovuti.
Je unafikiri unahitaji kuwa na tovuti? Angalia huduma zetu za wavuti. Huduma zetu za wavuti zitakuwezesha kukupa anuani ya tovuti, nafasi ya barua pepe na inakuwezesha kufungua tovuti kwa njia iliyo rafiki na simu yako katika muda mfupi kwa kupitia mifano iliyo tayari ya tovuti zilizosanifiwa.