Mawazo mengi ya sasa juu ya mikakati ya biashara ndogo yamekuwa yakifuata mabailiko makubwa yanayotokana na Internet. Internet kwa kiasi kikubwa imebadilisha taswira ya biashara ndogo na hata kuwa biashara kubwa kabisa. Kiufupi internet imekuwa ndio njia rahisi ya kuunganisha biashara ndogo na mteja.

Internet sasa imekuwa na jukumu kubwa la kutangaza na kuuza bidhaa pamoja na huduma ulimwenguni kote kwa ajili ya kupata wateja wengi. Internet sasa ni kijiji cha ulimwengu na inatoa nafasi kwa wamiliki wa biashara kutumia uwanja huu kama sehemu ya matangazo ya biashara yao kwa gharama ndogo sana.

SOMA ZAIDI

Internet inawezaje kubadilisha biashara ndogo?

  1. Internet inaongeza ufanisi wa masoko (Increase market efficiency)

Matumizi ya internet yanaongeza ufanisi mkubwa katika suala zima la masoko. Internet inatumika kuunganisha watu na biashara kwa urahisi na haraka sana. Wafanyabiashara wengi sasa haijalishi wadogo au wakubwa hutumia internet kwa ajili ya kuboresha biashara za hasa katika kuongeza mauzo na kutengeneza jina la biashara (Branding). Hii inatoa nafasi kubwa ya kuwa na soko kubwa la kibiashara.

  1. Kwenye internet hakuna anayejua kuwa biashara yako ni ndogo

Kwa mfano, kama ndio mara ya kwanza mteja anaingia kwenye tovuti yako ya biashara yako, ni ngumu kufahamu biashara yako inajumuisha watu wangapi, mmoja, wawili, watatu au hata kama ni kampuni ya watu elfu moja. Mara nyingi wateja wao uangalia ufumbuzi wa tatizo la hitaji lao tu.

Kitu kikubwa unachopaswa kukifanyia kazi basi ni kama unatumia tovuti (website) hakikisha tovuti yako inajibu mahususi kwa wateja hasa pale anapokuwa anatafuta kupitia mtandao. Kuna msemo unaosema kuwa.

“kwenye mtandao hakuna anayefahamu kama wewe ni mbwa”

(“On the internet, Nobody knows you are a dog”)

  1. Internet imebadilisha mtindo wa manunuzi ya biashara

Mtindo wa manunuzi ya biashara sasa umebadilika. Internet imefanya mnunuzi si lazima akutane na mtu au si lazima atembelee duka la bidhaa. Mnunuzi sasa anaweza kupata bidhaa yake pale alipo. Kupitia internet mteja anaweza kuagiza bidhaa na kuipata kwa muda uliokadiriwa pasipo kutembelea duka au ofisi husika.

Kupitia mambo hayo matatu, ni wazi internet kwa kiasi kikubwa imebadilisha kabisa taswira ya biashara ndogo. Kwa muda mrefu sasa Deep Media Tanzania imekuwa ikishugulika na wafanyabiashara wadogo ambao walikuwa wanakosa masoko kwa ajili ya kuuza bidhaa  na hata huduma zao. Deep media imewasaidia na kufanikiwa kuwa na soko pana la biashara zao.

Karibu Deep Media nawe tukusaidie kwa lolote linalohusu biashara, iliyo mpya na hata ya zamani. Wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA au kwa kupiga simu nambari

0758 259 234