Umeshawahi kujiuliza wamiliki wa biashara huwa wanatafuta nini kila siku? Kama haufahamu basi ni vitu vitatu tu,jinsi ya kuongeza mauzo (How to increase sales?), kuongeza ufanisi katika biashara (To improve effiency) pamoja na kutengeneza wateja watiifu kwenye biashara.

Hivyo ndivyo vitu vikuu vitatu ambavyo wafanyabiashara wengi uzingatia katika kuendesha biashara zao za kila siku.

Mwisho wa siku yote hayo yanafanyika ili kuingiza pesa au kuongeza mapato ili kutengeneza ustaswi wa maisha ya kila siku.

SOMA ZAIDI:

Ali Ispahany ni mtaalamu wa masuala ya kijamii na ni mkurugenzi wa makampuni yanayojihusisha na utengenezaji wa Apps mbalimbali za simu za mkononi. Alifanya utafiti wa kibiashara hasa kupitia biashara ndogo ndogo kama vile kumiliki maduka ya nguo kwa kuangalia maeneo hayo matatu.

  • Jinsi ya kuongeza Mauzo (How to increase sells)
  • Kuongeza ufanisi katika biashara (How to improve Effiency)
  • Jinsi ya kujenga wateja watiifu kwenye biashara (How to build loyal customer base)

Katika utafiti wake aligundua kuwa maeneo hayo matatu ni muhimu sana katika kukuza biashara. Hivyo alikuja na ufumbuzi wa matumizi ya Apps kama njia sahihi ya kuongeza mauzo, ufanisi pamoja na kutengeneza idadi kubwa ya wateja.

Ali Ispahany anasema matumizi ya Apps ni njia sahihi ya kufanya  biashara hasa kama utakuwa umejikita katika maeneo hayo matatu. Anasema kama unafikiria kutafuta kampuni ya kukutengenezea App ya kibiashara basi unapashwa kutafuta watu unaoweza kufanya nao kazi kwa ufanisi na wanaotambua mahitaji yako kama mmiliki wa Biashara.

Moja ya kampuni bora inayojishughulisha na utengenezaji wa Apps za simu katika Nyanja zote nchini Tanzania ni Deep Media. Ni kampuni ya Kitanzania inayohusisha jopo la wataalamu wenye ujuzi wa masuala ya Tehama, biashara na hata masuala ya kifedha.

Deep Media wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakusanya baadhi ya makampuni wenye uhitaji kwenye kujenga ufanisi, mauzo na hata kuongeza wigo wa wateja wake kupitia mfumo wa kidigitali.

Apps za simu zinaweza kufanya vitu vingi sana, inaweza kutumika kama njia ya kucheza michezo mbalimbali, kupata habari, kufanya masuala yako ya kibenki, kuiongoza nyumba yako au hata kampuni yako, kutumia kuwasiliana na wafanyabiashara wenzako hasa wadogo.

  • App ya simu (Mobile App) inawezaje kuongeza Mauzo?

Kwenye Apps ya simu kuna mipangilio mbalimbali na ya aina nyingi. Kila mpangilio (Program) umetengenezwa kwa ajili ya kumfanya mteja aweze kurudi tena. Wakati mwingine mtindo wa kutoa zawadi unatumika ili kumfanya mteja arudie mara kwa mara. Wakati mwingine mtindo wa zawadi  unaweza tengenezwa kwa mshindi kujipatia ofa kutokana na kusambaza ujumbe au picha kutoka kwenye App.

 

Lakini pia App ya simu inaweza kuongeza mauzo kwa kupitia njia zifuatazo

  1. Agiza kupitia simu (Mobile Order)

Unaweza kuongeza mauzo kwa kumfanya mteja apate nafasi ya kuagiza kitu kupitia App ya biashara yako. Hii inaonekana kuwa njia nzuri na rahisi kwa mteja kununua bidhaa popote anapokuwa.

  1. Kutuma jumbe za utambulisho kwa mteja (Push notifications)

Unaweza kutangaza vizuri biashara yako kama utakuwa na App ambayo itakuwezesha kutuma jumbe za utambulisho wa bidhaa mpya au ofa mbalimbali. Hata kutangaza punguzo la baadhi ya bidhaa zako kwa ajili ya kuongeza wateja.

  1. Kuwa na Jarida la kibiashara (Newsletter)

Kwenye App unaweza anzisha jarida la kibiashara  ili kumfanya mteja wako awe karibu na bidhaa yako.

  1. Rufaa ya kijamii (Social referral)

App yako ya simu inaweza kuwa na baadhi vipengele ambavyo vitampa mteja wako uwezo wa kusambaza ujumbe wako wa kibiashara kupitia mitandao ya kijamii.

  • App ya Simu (Mobile App) inawezaje kuongeza ufanisi?

Vipengele kama vya kuagiza vifaa vya madukani kama mapazia na vingine, kuagiza vyakula na vinywaji, huduma ya usafiri n.k huongeza ufanisi katika biashara hasa kwa wafanyakazi. Mfanyabiashara mdogo ambaye ameingia kwenye mfumo wa biashara yake kwa njia ya mtandao ataweza kuongeza ufanisi pamoja na kuongeza mauzo pia.

  • App ya Simu (Mobile App) inawezaje kutengeneza wateja?

Hiki ni kitu cha muhimu sana ambacho kila mfanyabiashara huwa analekilenga. Mteja ndio muhimili wa biashara yeyote ile. Kwa kutumia App ya simu unaweza ukadumisha mawasiliano kati ya mteja na biashara.

App inampa uwezo mteja wa kubadilishana taarifa na mfanya baishara kwa haraka na urahisi. Kadri mfanyabiashara anavyoweza kubadilishana taarifa na mteja kuna uwezekano mkubwa wa mteja kuwa balozi wa biashara au bidhaa Fulani.

App ya simu kwa sasa ni kama ilivyokuwa tovuti kwa miaka kadhaa huko nyuma. Ni wazi sasa matumizi yake yanazidi kukua siku hadi siku huku wafanyabishara wengi wakionekana kufaidika nayo.

Haujachelewa, unaweza sasa na wewe kuamua kutumia App ya simu (Mobile App) kwenye biashara yako ushuhudie matokeo chanya. Deep Media watakushauri na kukutengenezea App yenye kuendana na mahitaji ya biashara yako. Kwa msaada wasiliana nasi kupitia tovuti yetu HAPA.