Kuendesha biashara kunahitaji mbinu na mikakati kabambe ili kuweza kukuza na kuimarisha biashara husika. Hata hivyo katika uendeshaji wa biashara hatuna namna ya kuepuka kufanya matangazo ya biashara kwani ndio msingi wa kukuza mauzo ambayo kwa namna moja ama nyingine ndio chanzo cha kukua kwa biashara.

Hebu sikiliza mfano huu, Bwana Athumani na Bwana Charles wote ni wafanyabiashara wa nguo mbalimbali za dukani. Wote wanafanya biashara ya aina moja na huchukua bidhaa zao sehemu moja tofauti ni wakati wa kwenda kuchukua bidhaa tu. Bwana Charles yeye huwa anawahi sana kwenda kuchukua mzigo mpya. Tofauti na Bwana Athuman ambaye yeye kila siku kilio chake ni kuwa Biashara ni ngumu na mzigo huwa hauishi kwa wakati.

Kwa Bwana Charles yeye kwake mambo si haba, hata ukimuuliza kuhusu biashara yake jibu ni moja tu kuwa biashara yangu iko kwenye mzunguko wa kuridhisha. Baada ya kufanya uchunguzi kwanini ufanyaji wa biashara wa watu hawa wawili unatofautiana kimauzo.

Ndipo tukagundua kuwa Bwana Charles anawekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye kuitangaza biashara yake kupitia platform mbalimbali. Hili kwakwe linamsadia kuinua biashara yake tofauti na Bwana Athumani ambaye yeye ukaa tu dukani kwakwe na kusubiri wateja. Na pindi anapokosa wateja ndipo malalamiko ya ugumu wa biashara yake yanapokuja.

Ufanyaji wa Biashara unategemea mbinu na mikakati ya uendeshaji wa biashara yako. Umeshawahi kujiuliza kwanini wale ambao biashara zao hazitoki kwenye midomo ya watu wakati wote (biashara zinazotumia nguvu kubwa kujitangaza) zinazidi kukua kila siku?

Sasa katika kuliangalia hilo Deeep media tumefanya utafiti na kuja na suluhisho kwa wafanyabiashara hata wale wenye bajeti ndogo/ya chini ili kuwawezesha katika kukuza mauzo ya biashara zao.

Deep Media imekuletea mfumo wa Mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mteja na biashara husika kwa njia rahisi na ya moja kwa moja. Mfumo huu unaitwa Facebook Chatbots.

SOMA ZAIDI:

Facebook Chatbots ni nini?

Ni programu ya kompyuta au akili ya bandia ambayo inafanya mazungumzo kupitia njia za sauti au maandishi. Ni mpango wa mazungumzo unaohusisha wageni wa tovuti kujibu maswali, kutoa maelezo, kupendekeza bidhaa na kuwasaidia wateja kwenye safari yao ya ununuzi.

Faida za kutumia Facebook Chatbots

  1. Inamridhisha mteja kabla ya kufanya maamuzi

Kutumia Facebook Chatbots katika biashara yako ni kwamba unamfanya mteja aridhike zaidi na bidhaa au huduma zako. Wateja wanaounganisha tovuti yako wanaweza kuuliza maswali na kupata majibu mara moja. Ikiwa wana maswali ya bidhaa wanaweza kupata majibu wanayohitaji ili kukamilisha mauzo. Hii inaweza kuleta zaidi faida zako za biashara.

2. Inaokoa fedha katika biashara yako.

Facebook Chatbots ni rahisi mno. Haina gharama kama kuajiri watu wengine kwa ajili ya kufanya kazi ya huduma kwa wateja na masoko. Facebook Chatbots haina malipo ya gharama kama ambazo ungewalipa wafanyakazi.

3. Kuongeza idadi kubwa ya wateja wa biashara au huduma yako

Hii faida nyingine ya kutumia facebook Chatbots katika biashara yako. Inaweza kukusaidia kufikia watu wengi ambao wanaweza kuongeza wateja wako kwa haraka.

4. Inawezesha kushirikiana na mteja (Customer engagement)

Hapa hauhitaji kusema lolote, ni muhimu kuweka wateja wako karibu na wewe katika kushiriki kwenye brand yako. Kwa kufanya hivyo itakuwezesha kuitangaza brand yako kwa haraka na hatikaye kutenegeneza wateja kwa haraka na kwa idadi kubwa.

Hivyo basi kwa ajili ya kuongezea ufanisi katika biashara yako, Deep Media tunakuunganisha na mfumo huu moja kwa moja tena ka gharama nafuu sana. Wafanyabiashara wadogo wana nafasi kubwa sana katika kukuza biashara zao. Na hii ndio fursa pekee ambayo Deep Media wanakuwezesha. Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.