Pamoja na maendeleo na mwenendo wa teknolojia ya digitali ulimwenguni, Digital Market (Masoko ya kidigitali) yanatarajiwa kuchukua hatua kubwa katika siku zijazo. Makampuni na wafanyabiashara wengi ulimwenguni sasa wanawekeza bajeti zao katika kuangalia jinsi gani wanaweza kutumia fursa ya digital Platform.

Sio tu kwa sababu inagharimu kiasi kidogo cha fedha la asha bali uwezo wake wa kufikia idadi kubwa ya watu kwa muda sahihi, inafanya kuwa ndio sehemu pekee yenye kutengeneza mauzo ya hali ya Juu.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka ijayo soko la mtandaoni linaweza kushika atamu kwa kiasi kikubwa sana. Na ndio maana kwa kuzingatia hilo kampuni ya Deep Media imeamua kutafuta njia sahii ya kuwafanya wafanyabiashara wadogo wanufaike na maendeleo haya ya teknolojia kwa kukuza kuongeza mauzo yao Mara dufu. 

Njia mbadala kwa wafanya biashara wadogo

Wafanyabiashara wadogo amabao wanazungumziwa hapa ni wale ambao biashara zao ni za kawaida kama vile biashara ya nguo, simu, vipodozi, viatu n.k. Kiujumla hawa ziko katika ushindani wa hali ya juu kutokana na wimbi kubwa la watu wanaojishughulisha na biashara hizo. Hivyo basi Deep Media imeamua kutengeneza mfumo wa Facebook Chatbots ambao utamuwezesha mfanyabiashara kuzungumza na mteja ambaye tayari anahitaji bidhaa au huduma.

SOMA ZAIDI:

Facebook Chatbots ni nini?

Ni programu ya kompyuta au akili ya bandia ambayo inafanya mazungumzo kupitia njia za sauti au maandishi. Ni mpango wa mazungumzo unaohusisha wageni wa tovuti kujibu maswali, kutoa maelezo, kupendekeza bidhaa na kuwasaidia wateja kwenye safari yao ya ununuzi.

Hutumia lugha ya majadiliano/mdahalo kama njia ya kuweza kumshawishi mteja mapaka afikie hatua ya kuamua kufanya manunuzi ya bidhaa au huduma. Na hufanywa kwa njia ya mdahalo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja au kwa lengo la kutaka baadhi ya taarifa.

Je, Facebook Chatbots ni sawa na Facebook Messenger?

Jibu ni HAPANA. Facebook Messenger ni App inayotumika katika mawasiliano ya kawaida kupitia sanduku la Ujumbe. Ambayo inapatikana kwa kupakua kupitia andoid au Ios. Wakati Facebook Chatbots ni dhana (Tool) inayowezesha mawasiliano moja kwa moja na mteja na uunganishwa kwenye Facebook Messenger. kwa namna nyingine Facebook Chatbots ni huduma kwa mteja.

Faida za Facebook Chatbot katika digital Market

  1. Inamridhisha mteja kabla ya kufanya maamuzi

Kutumia Facebook Chatbots katika biashara yako ni kwamba unamfanya mteja aridhike zaidi na bidhaa au huduma zako. Wateja wanaounganisha tovuti yako wanaweza kuuliza maswali na kupata majibu mara moja. Ikiwa wana maswali ya bidhaa wanaweza kupata majibu wanayohitaji ili kukamilisha mauzo. Hii inaweza kuleta zaidi faida zako za biashara.

  1. Inaokoa fedha katika biashara yako.

Facebook Chatbots ni rahisi mno. Haina gharama kama kuajiri waru wengine kwa ajili ya kufanya kazi ya huduma kwa wateja na masoko. Facebook Chatbots haina malipo ya gharama kama ambazo ungewalipa wafanyakazi.

  1. Kuongeza idadi kubwa ya wateja wa biashara au huduma yako

Hii faida nyingine ya kutumia facebook Chatbots katika biashara yako. Inaweza kukusaidia kufikia watu wengi ambao wanaweza kuongeza wateja wako kwa haraka.

  1. Inawezesha kushirikiana na mteja (Customer angagement)

Hapa hauhitaji kusema lolote, ni muhimu kuweka wateja wako karibu na wewe katika kushiriki kwenye brand yako. Kwa kufanya hivyo itakuwezesha kuitangaza brand yako kwa haraka na hatikaye kutenegeneza wateja kwa haraka na kwa idadi kubwa.

Hivyo basi kwa ajili ya kuongezea ufanisi katika biashara yako, Deep Media tunakuunganisha na mfumo huu moja kwa moja tena ka gharama nafuu sana. Wafanyabiashara wadogo wana nafasi kubwa sana katika kukuza biashara zao. Na hii ndio fursa pekee ambayo Deep Media wanakuwezesha. Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.