Umeshawahi kujiuliza kwanini unatumia muda mrefu sana kufanya mahesabu, kusimamia shughuli za biashara/kampuni na hata kusimamia miradi ya biashara/kampuni yako?

ERP System ni mfumo pendwa unaoweza kuutumia katika kufanya shughuli zote hizo ndani ya biashara yako au kampuni yako kwa ufanisi zaidi. Mfumo huu unaweza kukusaidia katika kurahisisha utendaji kazi wako katika maeneo kadha wa kadha. Kwa kutumia ERP System, inaweza kukusaidia katika mambo yafuatayo:

JE, Utanufaikaje na mfumo huu wa ERP?

  1. Kupata ripoti kamili ya shughuli zako zote (Automatic Report)

Kwa wafanyabiashara mfumo huu unaweza kukupatia ripoti kamili ya faida na hasara kwenye biashara yako. Lakini pia mfumo huu una uwezo wa kutoa ripoti kamili ya shughuli zote na kukusaidia katika matumizi ya muda ambao ungetumia katika kuandaa ripoti.

  1. Mfumo wa ERP unakupa uwezo wa kiusalama kwa taarifa zako (Data Protection)

Mfumo huu unalinda taarifa zako tofauti na mfumo mwingine wowote wa utunzaji wa taarifa. Kwakuwa mfumo huu unatoa taarifa wenyewe pia una tabia ya kulinda taarifa hata kama kifaa chako unachotumia kutunzia taarifa kimepata hitilafu. Huwezi kupoteza taarifa kupitia mfumo huu. Kila taarif italindwa.

  1. Unasaidia katika usimamizi wa rasilimali watu (Human Resources Management)

ERP System inatumika pia katika kuendesha shughuli za uongozi pia katika upande wa rasilimali watu (wafanyakazi). Kupitia mfumo huu, afisa mwajiri hatokuwa na kazi kubwa sana katika kuwahudumia wafanyakazi. Mfumo huu unaweza kumsaidia katika utoaji wa,

  • Taarifa za Mishahara (Salary Component, Salary Slip &Salary structure)
  • Ruhusa za wafanyakazi (Leave Application & allocation)
  • Kodi za mishahara (PAYE)
  • Utoaji wa taarifa za kibenki (Bank Details)
  • Taarifa za wafanyakazi (Employee information)
  • Taarifa za malipo ya mishahara (Payrol Entry)
  1. Hurahisisha katika mchakato wa mahesabu ndani ya kampuni au Biashara (Accounting)

Kwa kutumia mfumo huu ni wazi unaenda kuondoa adha ya kutumia muda mwingi kufanya mahesabu ya ndani. Mfumo sasa unaondoa tatizo hilo na kukupa muda mwingi wa kufanya mambo mengine. Hurahisisha pia katika masula ya kukokotoa faida na hasara (Profit & Loss)

ERPNext tanzania

Deep Media Digital Agency kwa muda mrefu wameufanyia utafiti mfumo huu na kuwawezesha wafanyabiashara na makampuni mengi kutumia mfumo huu. Na sasa wengi wamenufaika nao. Tutembelee ofisini kwetu Mbezi beach chini, Bahari street, House No. 7, Plot 224 au taupigie kwa simu namba +255 758 259 234 tukuunganishe.