Umeshawahi kujiuliza kwanini unatumia muda mrefu sana kufanya mahesabu ya biashara yako? Au kufanya mahesabu ya kampuni yako? Au umeshawahi kujiuliza kwanini unatumia muda mrefu na hata kutumia nguvu kubwa katika kusimamia shughuli za biashara yako au kampuni yako? Ngoja niku jibu lenye suluhisho la tatizo lako.

Kwa zaidi ya miaka 5, kampuni ya Deep Media ikitumia jopo la watalaamu wake wa masuala ya Tehama (IT), imekuwa ikifanya utafiti juu mfumo upi unaweza kuongoza na kusimamaia shughuli za biashara yako au kampuni yako.

Utafiti huu ulikuja mara baada ya kugundua kuwa wafanyabiashara wengi na hata wamiliki wa makampuni mbalimbali wamekuwa wakitumia muda mrefu na nguvu kazi kubwa katika kuendesha biashara zao.

Mfumo wa ERP ndio suluhisho la tatizo linaloikumba makampuni mengi nchini. Kwa kutumia mfuMo huu kampuni au biashara inaweza kusimamia shughuli zake zote za kibishara na hata za ndani ya kampuni kwa urahisi zaidi.

SOMA ZAIDI:

 

Mfumo wa ERP ni mfumo gani? (Enterprise Resource Planning System)

Ni mfumo unaotumika katika kusimamia michakato ya misingi ya shughuli mbalimbali kama vile biashara na huduma, kwa kutumia progamu maalum ya kiteknolojia. ERP hujulikana kama programu ya usimamizi wa biashara

Faida ya kutumia mfumo wa ERP katika biashara au kampuni yako

1. Husaidia kusimamia shughuli zote za uongozi na rasilimali watu (HR)

Kwa kutumia mfumo huu wa kisasa katika biashara yako au kampuni yako, afisa rasilimali watu atakuwa na uwezo wa

•  kuweka ekodi za wafanyakazi katika nyanja zote tena kwa urahisi kabisa.

• Lakini pia meneja rasilimali watu atakuwa na uwezo wa kusimamia na kudhibiti malipo wafanyakazi (Pay roll). Ikiwa ni pamoja na kurekodi malipo yote kwa haraka zaidi.

• Rasilimali watu inaweza kudhibitiwa kupitia shughuli mbalimbali za nje na ndani ya kampuni. Kama vile ruhusa mbalimbali kama ruhusa za ugonjwa, uzazi (Martenity leave), dharura n.k.

2. Hurahisisha mchakato wa mahesabu ya biashara ya kampuni (Accounting)

Kupitia mfumo huu ambao ni mfumo pendwa kwa sasa katika shughuli mbalimbali za kibiashara. Unawezesha kurekodi masuala yote ya kifedha (mahesabu) kwa haraka na kwa urahisi.

Mfumo wa ERP unakupa fursa ya kurekodi mahesabu ya faida (profit) na hasara (loss) baada ya kuwa na ingizo katika biashara.

ERP inakusaidia kurekodi mauzo na manunuzi kwa urahisi zaidi tofauti na mifuo mengine ambayo imekuwa ikitumika kwa nyakati za zamani.

3. Hurahisisha katika kujua kiasi cha bidhaa kinachoingia na kutoka (Inventory)

Katika mfumo huu, kwenye biashara utakusaidia kujua kiasi halisi cha bidhaa ulichokuwa nacho kwenye ghala. Pia kukusaidia katika kujua mzigo kiasi gani unaingia na kutoka kwa urahisi zaidi.

Husaidia pia katika kusimamia oda ya manunuzi (Purchasing order) na kusimamia mauzo kwa urahisi zaidi.

Pia katika biashara ERP itakusaidia katika kudhibiti na kusimamia malipo ya bidhaa zako kwa urahisi ili kuepuka hasara ianyoweza kujitokeza.

4. ERP inasaidia kusimamia shughuli za miradi mbalimbali ya kampuni.

Katika biashar yeyote au kampuni kunakuwa na miradi mbalimbali inayotazamiwa kuendeshwa. Mara nyingi miradi inakuja na shughuli mbalimbali. Mfumo huu utasaidia kusimamia kazi zote zinazotokana na miradi hii kwa urahisi zaidi.

5. Mfumo pendwa kwa wafanyakazi

Kwa kutumia mfumo huu mfanyakazi anaweza kujiendesha mwenyewe kwa kufanya kazi bila hata kutumia mlolongo mrefu. Kwa mfano mfanyakazi anaweza kuomba ruhusa ya dharura au ruhusa ya jambo Fulani moja kwa moja kupitia program hii. Na kisha atapokea uthibitisho haraka kupitia mfumo huu.

Lakini pia mfumo huu utamfanya mfanyakazi atambue wajibu na shughuli anazopaswa kufanya kwa kipindi Fulani kwa haraka kwa kutumia mfumo huu.

Lakini pia mambo yote yanayohusu malipo kama vile stakabadhi ya malipo ya mshahara na mengineyo atayapata moja kwa moja kupitia program hii.

Hivyo basi mfumo huu kwa njia moja ama namna nyingine umekuwa suluhisho la makampuni mengi ambayo yalikuwa yanapata shida katika utendaji. Mfumo huu unakupa fursa ya kuendesha biashara yako na hata kampuni yako pasipo kuwa na mlolono mrefu huku ukitumia mud mfupi sana.

Kwa msaada zaidi na jinsi ya kupata mfumo huu ili nawe uwe mmoja ya watu ambao wamefanikiwa tafadhali wasiliana nasi Deep media kwa kubonyeza HAPA.