Mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa hususani mtandao wa instagram. Licha ya matumizi makubwa ya mtandao huu bado idadi ndogo tu ya watumaiaji wanaotumia kama njia ya kukuza biashara na kuongeza kipato.

SOMA ZAIDI: Biashara ya Mtandaoni inavyoweza kukuingizia kipato

Kutumia mitandao ya kijamii kuongeza kipato

zingatia:

Mtandao wa Statista unaripoti kuwa idadi ya watumiaji wa instagram inapanda siku hadi siku. Mpaka kufikia mwezi Juni, 2018 zaidi ya watu billion 1 walikuwa wanatumia mtandao huo wa instagram.

Nchini Tanzania takwimu za kimtandao zinaonyesha matumizi ya mdahalishi (Internet) nchini Tanzania yanaongezeka siku hadi siku. Ripoti ya mawasiliano ya mwezi Juni, 2018 ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha Tanzania pekee ina zaidi ya watumiaji wa internet millioni 22.

Ni Wazi takwimu hiyo inatoa fursa kubwa katika nyanja ya kibiashara katika namna ya kukuza biashara na kuongeza kipato kwa kutumia mtandao.

Njia 7 za kutumia mtandao wa Instagram kukuza biashara yako

  1. Onyesha unachokifanya katika njia ya Ubunifu:

Zingatia sana katika kutoa ufumbuzi wa tatizo kutokana na bidhaa/huduma yako na sio kulenga bidhaa unayoiuza. Hii itaongeza thamani kwa wateja wako na kukuza biashara yako. Kama unatoa huduma basi jikite kuonyesha njia unazozitumia kutoa huduma yako.

  1. Tengeneza Wasifu(profile) wenye kuleta tija

Unaweza ukawa unajihusisha na biashara mbalimbali katika kampuni/binafsi. Haupaswi kumulika sana shughuli zote unazozifanya jaribu kumulika katika jambo moja ambalo ni la muhimu na kubwa sana katika kukuza biashara au huduma unayoitoa.

  1. Waonyeshe wateja wako upatikanaji au uzalishaji wa bidhaa/huduma zako.

Mara nyingi wateja huwa wanakuwa na shahuku ya kutaka kufahamu kuhusu wapi unazalisha au unazitoa bidhaa zako, hivyo unapaswa kuwaonyesha wateja wako mzunguko mzima wa upatikanaji wa bidhaa zako, hii inaongeza thamani ya bidhaa zako. Itakusaidia pia kukuza biashara yako kwa kasi zaidi.

  1. Dumisha mawanda ya bidhaa/huduma yako kwa #hashtag

Matumizi ya Hashtag yanasaidia katika kuongeza idadi ya wateja utakaowafikia katika eneo kubwa sana. Hii unaweza kuitumia kwa njia kama kufanya kampeni maalumu ya kukuza bidhaa/huduma yako.

 

  1. Shirikiana na baadhi ya taasisi au kampuni nyingine za kijamii

Mtandao wa Instagram ni moja ya mtandao wa kijamii wenye nguvu sana hasa katika kutengeneza wafuasi kwa pamoja. Hata kama hauna ushirikiano wowote wa kibiashara na taasisi zozote za kijamii jitahidi kutengeneza ushirikiano katika kufanya kampeni za kusaidia jamii husika yenye uhitaji, hii inaweza kuongeza thamani ya kampuni yako ama kukuza biashara yako.

  1. Jenga maatajio mazuri kwa wateja na kutoa Ofa

Kama unataka kukuza biashara yako, daima unapaswa kumfanya mteja wako awe na shahuku ya kukufuata kwenye mtandao wako mara kwa mara. Hii unaweza kuifanya katika njia ya kuwapa maudhui ambayo wanapaswa kuyajua kwa wakati. Taarifa kama kuhusu bidhaa mpya, huduma mpya, matukio au matamasha na hata jambo lolote geni.

  1. Changanua mafanikio yako na simamia katika hayo

Bila ya kuchukua hatua za kurudi nyuma na kufanya uchanganuzi wa kipi kimefanya kazi katika mipango yako na kipi hakikuenda sawa utakuwa unacheza mchezo wa kubashiri.

Ukweli ni kwamba unapaswa kuchanganua ukurasa wako wa instagram kwa kuangalia wangapi wanaokufuata, wanaojihusisha na bidhaa zako pamoja na wanaotazama bidhaa zako ili uweze kukuza biashara yako.

Kwa kutumia njia hizo unaweza kutengeneza idadi ya wateja wengi wenye matakwa na bidhaa au huduma yako. Lakini pia kuna faida nyingi sana za kutumia instagram kama sehemu ya kukuza biashara yako.

Faida za kutumia Instagram kwenye Biashara yako

  1. Instagram inatoa nafasi ya kueleza kwa undani jambo Fulani kama vile stori ya vitu au watu mashuhuri, watumiaji wengi wa instagramu wanapenda stori.
  2. Madhui ya picha/Video ni muhimu sana katika suala la kutafuta masoko. Wateja uamini katika kile wanachokiona.
  3. Kupitia Instagram unaweza kuwafikia idadi kubwa ya watu
  4. Ni sehemu maridhawa ya kushirikiana na wateja wako kuliko sehemu yeyote
  5. Ni sehemu sahihi ya kuweza kupata mrejesho kamili na maono ya biashara yako
  6. Instagram inakupa nafasi ya kujua kuhusu washindani wako

Wengi wamekuwa na uoga mkubwa pamoja na maswali mengi wanawezaje kutengeneza wateja wengi na hatimaye kukuza biashara zao. Ni rahisi tu BONYEZA HAPA kwa msaada wowote kuhusu biashara mtandoni