Katika sekta biashara ya inaonekana kama daima huwa tuangahaika sana kutafuta wateja wapya. Wengi wetu tunapigana ili kuhakikisha matangazo yetu, mabango na bei zote “hulia” zinagonga vichwa vya wateja wetu ili kuvutia biashara.

Lengo hilo la kutafuta wateja wapya ili kuongeza mauzo ni jambo la uhakika na muhimu. Lakini, wakati huo huo, inaweza kutuletea maumivu. Hivyo basi lengo letu linapaswa kuwa juu ya wateja waaminifu (Loyal Customers)  ambapo ni  asilimia 20 ya wateja wetu ambao kwa sasa ni wateja wetu bora.

Katika biashara, wazo hili la kuzingatia wateja bora zaidi inapaswa kuonekana kama nafasi endelevu. Ili kuelewa vizuri maana ya nadharia hii na kukabiliana na changamoto ya kujenga uaminifu wa wateja. Tunahitaji kuwachambua wauzaji katika aina tano kuu za wateja.

SOMA ZAIDI:

 Mteja (Customer) ni nani?

Mteja ni mtu au mpokeaji wa huduma, bidhaa au wazo fulani lililopatikana kutoka kwa muuzaji au msambazaji kupitia miamala ya kifedha au namna nyingine ya kuonyesha thamani. Au tunaweza kusema mteja ni mtu ambaye ununua bidhaa au huduma kutoka kwenye duka fulani au ofisi husika.

Aina za Wateja.

1.     Wateja Waaminifu (Loyal Customers)

Hawa ni aina ya wateja ambao hawawakilishi hata zaidi ya asilimia 20 ya wateja wetu, lakini hufanya zaidi ya asilimia 50 ya mauzo yetu.

Kwa kawaida, tunahitaji kuwasiliana na wateja hawa mara kwa mara kwa simu, barua, barua pepe, mitandao ya kijamii, nk. Watu hawa ndio ambao wanaweza na wanapaswa kuathiri maamuzi yetu ya kununua na bidhaa. Hakuna kitu kitakachofanya wateja waaminifu kujisikia vizuri zaidi ya kukipa thamani kiasi au kitu watakachokitoa.

2.     Wateja wa Kiasi (Discount Customers)

Hawa ni aina ya wateja ambao ununua bidhaa na huduma kwenye maduka yetu lakini wanafanya maamuzi yao kulingana na kiasi cha gharama au bei za bidhaa zilizoshushwa.

3.     Wateja wenye kushawishika (Impulse Customers)

Hawa ni aina ya wateja ambao wanakuwa na uamuzi usiopangwa wa kununua bidhaa au huduma, mara nyingi huvuta na hisia au kuona bidhaa au kushawiushika na tangazo la bidhaa husika. Wao ununua kitu pale wanapokiona kuwa kitu kile ni kizuri.

Hakika hawa ndio aina ya wateja ambao kila mmoja wetu angependa kuwahudumia. Kwa sababu maamuzi yao hufanywa kutokana hisia baada ya kuona uzuri wa kitu.

 4.     Wateja wa Mahitaji Maalum (Need-Based Customers)

Wateja wa aina hii huwa wanaendeshwa na mahitaji maalum. Wanapoingia kwenye duka, wataangalia kuona kama wanaweza kuwa na hitaji lao. Ikiwa watakosa, wataondoka mara moja. Wananunua kwa sababu mbalimbali kama vile tukio maalum, mahitaji maalum, au kiwango cha bei fulani. Wanaweza pia kuwa wateja waaminifu ikiwa wanahudumiwa vizuri.  

Ni muhimu kukumbuka kuwa wateja wa aina hii unaweza kuwapoteza kutokana na biashara za mtandaoni. Hivyo basi ili kuondokana na tishio hili, utoaji wa huduma nzuri unahitaji hasa kwa wauzaji

5.     Wateja washagazi (Wandering Customer)

Hawa ni aina ya wateja ambao hawana uhakika wanataka kununua.Hawana haja maalum au matakwa halisi katika akili yao wakati wanaingia kwenye duka. Badala yake, wanataka hisia ya uzoefu na  mwitikio wa jamii.

Wanaweza wakawa wengi na kutengeneza kiasi kikubwa cha trafiki kwenye kampuni au maduka huku tukishuhudia asilimia ndogo kati yao ufanya maamuzi.

Wateja ni kiungo muhimu sana katika biashara yoyote. Ili kuelewa tabia ya wateja na kuboresha rasilimali kwa wateja mbalimbali ili kuzalisha faida kubwa, ni muhimu kuwa na uwezo wa kutambua na kuchanganua aina tofauti za wateja. Kwa kuelewa vizuri aina tofauti za wateja, biashara inaweza kuwa vyema katika kuendeleza mikakati ya mafanikio.

Biashara yeyote inahitaji mipango na mikakati. Unaweza sasa kuboresha biashara yako kwa asilimia zaidi ya 80% kupitia digital platform na Deep Media. Bonyeza HAPA kwa msaada zaidi.