Kila biashara ambayo hutumia Social Media (Mitandao ya kijamii) katika kujitangaza inahitaji mpango kazi wake maalum. Bila kuwa na mpango kazi wowote wa social media kwenye biashara yako, kampuni yako inapoteza muda wake tu.

Je, Ungependa kuajiri mtu wa kutengeneza picha yeyote au bango lenye kujenga ishara kubwa kwa biashara yako na kisha kuliweka kwenye barabara yeyote ile? Hivyo ndiyo unavyofanya wakati unapotangaza kwenye social Media (Mitandao ya kijamii) ukiwa hauna mpango kazi.

Kama vyombo vya habari vinginevyo, kutumia social Media kuunganishwa na wateja wako na kuwashawishi kuchukua hatua inahitaji mpango kazi, muda na fedha ili  kuweza kutekeleza hilo.

Kwa bahati nzuri, huna haja ya kutaka kujua jinsi ya kutumia zaidi ya platform kumi na nne za social Media (Mitandao ya kijamii) ili kuunda mpango kazi wake, au kutenga siku nyingi. Unachotakiwa kufanya ni kufanya maamuzi haya matano.

SOMA ZAIDI:

Mambo ya kuzingatia katika kuandaa mpango kazi wa Social Media

1.   Ni Mtandao gani wa kijamii (Social Media) unafaa zaidi kwa ajili ya biashraya yako?

Mojawapo ya ushauri bora zaidi kuhusu Social Media katika kujua mwelekeo wa biashara yako ni kujua Mtandao gani ni bora zaidi kwa biashara yako. Biashara nyingi na makampuni mengi hawawezi kutumia Mitandao ya kijamii mingi kwa biashara zao. Hivyo ni muhimu kuzingatia katika uchaguzi wa mtandao mmoja ambao utakuwa maridadi kwa biashara yako.

Je, unawezaje kujua ni Mtandao upi bora kwa biashara yako?

Hili kuweza kujibu swali hili kwanza unapaswa kujua ni mtandao upi ambao wateja wako hutumia mara kwa mara. Hili kujua hilo unapaswa kufanya utafiti mdogo kwa wateja wako ili kuweza kujua. Unaweza kufanya utafiti kupitia mitandao yako ya kijamii lakini pia unaweza kufanya utafiti kupitia tovuti yako.

Hivypo basi ni vyema kujua mtandao upi ni bora kwenye biashara yako kabla ya kutengeneza Mpango kazi wako.

2.   Nini malengo ya Mtandao wako wa kijamii?

Sasa kwa kuwa umeshachagua ni Social Media ipi inafaa katika biashara yako. Hapa unahitaji kujua nini hasa kusudi lako la kuamua kutumia mtandao huo. Social Media kwa biashara inaweza kutumiwa kwa malengo sawa na marketing channel yeyote nyingine. Kwa mfano, unaweza kutumia Social Media kwa:

  • Kwa ajili kuongeza watumiaji wa bidhaa au huduma yako
  • Ili Kuongeza Mauzo ya biashara yako
  • Uboresha jina la biashara yako
  • Uongeza Traffic kwenye tovuti yako au ukurasa wako
  • Mikakati ya Kutangaza bidhaa mpya au huduma
  • Kutoa huduma kwa wateja

3.   Utapimaje mafanikio ya Social Media yako?

Hii ni hatua ambayo wamiliki wa biashara mara nyingi huwa hawaizingatii wanapokuwa wanaandaa mpango kazi wao wa Social Media, lakini ni moja ya hatua muhimu zaidi.

Kwa kawaida, mafanikio ya Mitandao ya kijamii yanapaswa kupimwa sawa na jitihada nyingine zinazotumika za masoko; Hapa tunazungumzia,

  • Gharama (Cost)
  • Marejesho (Return)
  • Uwekezaji (Investment)

Zipo njia mbalimbali zinazotumika katika kujua mafanikio ya Social Media inategemea na social Media ipi unatumia. Kwa jina moja tunaita Analytics. Ukiwa na Tovuti unaweza kutumia Google Analytics, ambapo inakuwezesha kufuatilia na kuchambua tovuti mbalimbali, data za Simu na data za Social Media.

Hii itakuwezesha kujua utendaji kazi wa Social Media yako kwakuwa itaweza kukupa ripoti kamili ya data zote.

4.   Bajeti yako ya Social Media ni ya kiasi gani?

Zaidi ya 50% ya wafanyabiashara wengi wadogo huwa na bajeti ndogo hasa kwenye suala la Masoko. Lakini wengi wanashindwa kujua wanaweza kutumia kiasi hicho kidogo katika kuwekeza katika Social Media ambako wanaweza klutengeneza idadi kubwa ya wateja.

Kabla ya kuandaa mpango kazi wako unapaswa kujua bajeti yako na hii itatokana na kujua nini hasa malengo yako. Kwanza angalia malengo yako kisha andaa bajeti yako.

Mfano unaweza kuchagua kutumia Facebook kufanya kampeni ya kutengeneza wateja (Leads Generation). Unahitaji kuwa na bajeti

5.   Nani atahusika kutekeleza mpango kazi uliouandaa?

Hapa tunazungumzia mtu ambaye atahusika kwa jambo linaloendelea kwenye Mitandao ya kijmaii. Unaweza wewe mwenyewe kupanga muda wako kulingana na malengo yako au unaweza kuamua kuajiri mtu maalum ambaye anaweza kufikia malengo.

Makampuni mengi sasa yanaajiri watu maalumu wa kitengo cha Social Media ambao ndio wenye jukumu la kutekeleza mipango yote. Lakini wengine uajiri makampuni maalum yanayoijihusisha na kuendesha Mitandao ya kijamii mbalimbali. Hawa ni wataalamu waliobobea kwenye idara hiyo.

Matumizi ya Mitandao ya kijami kwa sasa ni vigumum kuepuka. Idadi kubwa ya watu sasa hutumia social Media huku idadi ya wanaotumia televisheni na radio kwa njia ya kawaida ikipungua. Hii inatengeneza wigo sasa wa nkutangaza  biashara yako kwa bajeti ndogo tena ukiwa hata umejifungia ndani kwako.

Kampuni ya Deep Media Tanzania imejidhatiti katika kuborehsa mazingira yote yanayohusu biashara hasa kwa kutumia platform ya kidigitali. Unaweza kutangaza biashara yako au hata kutengeneza wateja nasi kwa kuwasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA au kwa kupiga simu Nambari 0758259234