Matumizi ya Business Email yamekuwa makubwa mno sasa. Na hatimaye kuwa chombo kinachotegemewa katika kutambulisha jina la biashara pamoja na kujenga uaminifu. Pamoja na ukuaji mkubwa wa Mitandao ya digitali kama vile mitandao ya kijamii, bado Email inabaki kuwa ndio njia pekee ya mawasiliano ya kibiashara.

Biashara hutuma maelfu ya Email katika kufanya kazi zao muhimu za kibiashara. lakini licha ya matumizi makubwa ya barua pepe za biashara (Business Emali), bado kuna mashirika mengi ya hutumia huduma za bure za kuhudumia barua pepe kama Gmail, Hotmail, au Yahoo kwenye biashara zao.

Hata hivyo, akaunti hizi za barua pepe huwapa ID zao kama hizo za barua pepe (yahoo, gmail hotmail). Kwa hili, wanahitaji kupata huduma ya barua pepe ya biashara.

Business Email/ barua pepe ya biashara ni nini?

“Business Email” ni barua pepe ambayo inatumika hasa kwa ajili ya biashara. Kwa kawaida, anwani ya barua pepe ya biashara inajumuisha jina la kampuni ndani yake. Jinalako/info@jinalakampuni.co.tz (info@deepmedia.co.tz/john.maliki@deepmedia.co.tz ).

Njia hii ya kitaaluma ya kutuma barua pepe ya biashara pia itatumika kama aina ya matangazo kama jina lako la biashara litaonekana kwenye kila mawasiliano yako yatakayouhusisha barua pepe.

Kila wakati unapotuma barua pepe, mpokeaji atakumbushwa wewe ni nani na atajua mara moja kampuni ambayo unawakilisha, hata kama haujawahi kukutana nawe, ambayo ni habari njema kwa biashara ndogo ambayo inajaribu kujenga ufahamu wa bidhaa.

SOMA ZAIDI:

Je, unajua faida za kutumia Business Email?

Anwani ya barua pepe ya biashara ina jina la kampuni ndani yake kama employename@companyname.com. Kitambulisho hiki cha barua pepe cha kitaaluma sio tu kuanzisha mamlaka ya mtu kutenda kwa niaba ya kampuni lakini pia hufanya kama tangazo la kampuni kwa sababu jina la biashara linabakia kuonekana na mawasiliano yote ambayo wafanyakazi hufanya. Kuna faida nyingi zaidi za akaunti ya kumiliki barua pepe ya biashara. Faida hizo ni kama,

  1. Inaonyesha jinsi unavyoweza kusimamia biashara yako

Hii ni nafasi ya kwanza ya kutengenza ushawishi kwa mteja wko. Unapowasiliana na mteja wako kwa mara ya kwanza hasa wateja wapya kupitia Business Email/barua pepe ya biashara kama vile info@deepmedia.co.tz itaakisi biashara yako vizuri zaidi kuliko kutumia johnexaurd41@gmail.com au john345@yahoo.com. Kuwa na Email yako iliyounganishwa kwenye domain yako mwenyewe huleta weledi katika biashara yako. Ingeweza kuwa john@deepmedia.co.tz au john.maliki@deepmedia.co.tz

  1. Inajenga uaminifu (It builds trust)

Utafiti mbalimbali umegundua kwamba anwani ya barua pepe ya biashara (Business Email) husaidia kujenga uaminifu kwa wateja. Kuwa na barua pepe/Email na tovuti/Website zilizounganishwa pamoja inaonyesha kuwa ni jinsi gani uko makini na biashara yako na itakusaidia kujenga uaminifu kutoka kwa wateja wanaotarajiwa au washiriki.

Lakini sio tu kujenga uaminifu, barua pepe ya biashara (Business Email), inaweza pia kutumika kama chombo cha masoko ili kuendesha trafiki zaidi kwenye tovuti yako.

  1. Inasaidia kulinda data Muhimu za biashara yako

Barua pepe nyingi za kijamii ni rahisi kuzidukua, na kufanya taarifa za biashara yako kuwa katika hali ya hatari. Taarifa zako za siri za biashara yako zinaweza kuwa mikononi mwa wadukuzi. Kulingana na hali ya biashara yako ya matumizi ya Email za jumuiya, suala la faragha/ usiri wa taarifa za biashara yako linaweza kuwa ni ndoto.

  1. Hauwezi kuitangaza kampuni nyingine badala ya kwako

Jina la biashara yako daima linapaswa kuwa juu na kwenye vichwa vya watu wengi hasa unapokuwa unahusisha saula la masoko. Ikiwa utakuwa unatumia barua pepe/Email ya @yahoo.com au @comcast.net au @ gmail.com, wewe utakuwa unahusika kuyatangaza makampuni hayo. Tofauti na utakaokuwa unatumia domain yako kwa mfano, info@deepmedia.co.tz.

  1. Inaweza kutumika kama utambulisho wa kampuni/biashara.

Unapokuwa na barua pepe yenye domain ya jina la biashara yako inakuwa rahisi hata kwa wateja wako kutambua kwa haraka. Mfano ukitumiwa barua pepe na mtu wa masoko wa kampuni ya Deep Media, atakapotuma kupitia barua pepe binafsi itamuhitaji maelezo ya utambulisho tofauti angetumia bariua pepe ya kampuni. Yaani john345@gmail.com na info@deepmedia.co.tz

Kila wakati unapotuma barua pepe, mpokeaji atakumbushwa wewe ni nani na atajua mara moja kampuni ambayo unawakilisha, hata kama haujawahi kukutana nawe, ambayo ni habari njema kwa biashara ndogo ambayo inajaribu kujenga ufahamu wa bidhaa.

  1. Inasaidia kulinda Mawasiliano ya ndani ya kampuni

Business Email zinakuwa zinasimamiwa na kampuni husika, ambapo mawasiliano yote ya ndani yanapitia kwenye email maalumu ya biashara. Mfano john Maliki wa deep media (john.maliki@deepmedia.co.tz). Hii ni rahisi kudhibiti hata pale mfanyakazi anapokuwa ametoka kazini. Kampuni inaweza kusitisha na mawasiliano ya kampuni yakabaki ndani ya kampuni.

Hivyo basi, business Email ndiyo njia kuu ya mawasiliano kwa biashara yeyote ile yenye lengo la kufika mbali, na labda ni muhimu zaidi. Hii ndiyo sababu Business Email inaweza kuwa njia nzuri ya kukuza biashara yako.

Deep Media Tanzania (Digital Media Agency) wanakusudia kutimiza ndoto ya biashara yako kwa kukutengenezea Email rasmi kwa ajili ya biashara yako ili uweze kuingia sasa kwenye soko la ushindani. Tembelea kurasa zetu mbalimbali na kwa mawasiliano bonyeza HAPA, Au tupigie 0758259234