“Tunampa kipaumbele mteja kwanza!” (We put the Customer First). Bila shaka umewahi kusikia maneno haya kabla, na pengine kutoka kwenye kampuni zaidi ya moja. Neno hili ni ahadi ya msingi katika taarifa nyingi za ujumbe, vichwa vya habari vya tovuti, na umekuwa wimbo wa timu za huduma kwa wateja kila mahali. Leo, ni vigumu kupata kampuni isiyosema, “tunampa kipaumbele mteja kwanza” katika sehemu fulani ya ujumbe wao.
Lakini, jambo gumu hapa la kujiuliza ni kuwa kampuni ngapi kati yao wanaenda ndani zaidi ya ujumbe huo wa masoko na kwa kweli kuchukua hatua muhimu za kuweka wateja wao mbele kwanza?
Kulingana na utafiti mpya wa HubSpot unaonyesha kuwa ni kampuni chache tu ambao uenda mbali zaidi. Utafiti umegundua kwamba 42% ya makampuni huwa hawafanyi utafiti wa hitaji la wateja wao pamoja na kupitia na kukusanya maoni yao.
Sasa swali la kujiuliza hapa ni kuwa, Je! Kampuni yako inawezaje kusema kuwa inawapa kipaumbele sana wateja wake ikiwa haitumii jitihada zozote katika kusikiliza nini wateja wako wanasem na nini wanahitaji kusema?. Ukweli ni huu, ingawa biashara nyingi zinadai kuwa “Mteja kwanza”, lakini hazichukui hatua za kuwa tayari kwa wateja wao.
Hata hivyo takwimu hizo zinadai kuwa ni 12% tu ya wateja ndio wanaoamini kuwa biashara zinazotoa ujumbe wa kuwa “mteja kwanza” huwa zinafanya jitihada za kutekeleza azma hiyo.
Utafiti wa mawakala wa huduma ya wateja duniani jinsi wanavyotumia data za wateja.
Utafiti katika sehemu kubwa, Biashara nyingi zina nia njema wakati wanasema ni “mteja kwanza,” lakini husema tu kuliko kufanya.
Ikiwa unataka kujenga biashara yako iwe karibu na wateja wako, kuna hatua kadhaa rahisi ambazo unaweza kuchukua ili kuanza.
SOMA ZAIDI:
- Je, unajua faida ya kutangaza biashara kupitia mitandao ya kijamii?
- Aina ya wateja wa biashara yako na tabia zao
- Kwanini utumie Facebook Kutangaza Biashara yako?
- Jinsi mtandao unavyoweza kuibeba biashara yako
HATUA ZA KUCHUKUA ILI BIASHARA YAKO IWE KARIBU NA WATEJA
-
Fanya uchunguzi kwa wa wateja wako
Kufanya uchunguzi ni jambo thabiti katika biashara nyako. Na hii utokana na kujali na kupitia maoni mbalimbali kutoka kwa wateja wako ili kuweza kujua nini wateja wako hupenda.
-
Tengeneza kanuni za wateja
Wateja wanajitegemea zaidi, wenye subira, na hawana imani zaidi na biashara. Ni rahisi sana kusambaza taarifa hasi za biashara kwa kiasi kikubwa na wanaweza kumshirikisha na kumchagua moja ya mshindani wako.
Kanuni ya Wateja inaelezea kuweka pamoja kanuni na imani juu ya jinsi ya kujenga kampuni ambayo wateja hupenda. Sio kuhusu unayouza, lakini jinsi unavyouza. Ni juu ya kufanya wateja wako wawe na mafanikio zaidi, kujenga mahusiano kwa kufanya jambo sahihi.
-
Kutafiti jinsi makampuni mengine yamekua kwa mafanikio na mawazo/maoni ya wateja
Kama biashara unapaswa kujifunza kupitia wengine waliofanikiwa. Wapo ambao hutumia mawazo ya wateja katika kuboresha biashara zao. Na hiyo ndio njia pekee ya mafanikio ya biashara zao. Kuzingatia wateja wako, biashara yako itaongezeka vizuri.
Kuimarisha mtazamo wako kwa wateja na jinsi wanavyohisi kuhusu kampuni / bidhaa huduma yako ni muhimu kwa ukuaji wa biashara yako. Uchunguzi uligundua kuwa 69.5% ya makampuni wanakiri kwamba kupitia kurasa mbalimbali, mitandao ya kijamii au hata njia ya mdomo kunaweza kukuza biashara
Hivyo basi katika kipindi hiki ambacho mtandao ndio umekuwa njia kuu ya kukuza biashara, sasa ni busara kwa wafanya biashara kupitia mawazo mbalimbali ya kwenye kurasa zao. Wateja huwa wanapenda kuacha mawazo na maoni yao kupitia mitandao mbalimbali.
Kwa msaada zaidi jinsi ya kutumia digital platform kukuza biashara yako wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA au kwa kupiga simu moja kwa moja kupitia namba 0689055415